Habari za Punde

Othman Miraji astaafu DW Redio Ujerumani





Baada ya miaka 35 ya utumishi wa uaminifu katika Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani, Othmani Miraji Ijumaa, 12.10.2012, ilikuwa siku yake ya mwisho kazini kama Mhariri Mwandamizi. Wafanyakazi wenzake, wakiongozwa na Mhariri Mkuu wa DW, Bibi Ute Shaeffer, na pia mkuu wa matangazo ya Kiswahili, Bibi Andrea Schmidt, walimfanyia karamu murua ya kumuaga na kumtakia kila la heri na afya njema katika maisha yake ya baadaye. Pia walisifu mchango mkubwa alioutoa katika kuifanya DW iwe kiunganisho cha kupata habari za kuaminika na motomoto kutoka duniani kote na katika kuikuza lugha ya Kiswahili. Othman Miraji alijiunga na DW akitokea Idara ya Kunasa Matangazo ya BBC (Monitoring Service), Nairobi, Kenya, mwaka 1977 ambako alitumika kwa miaka saba.

4 comments:

  1. Mmoja kati ya watangazaji bora sana walionivutia sana bila kusahau kipindi cha darubini uchambuzi wa kisiasa wa kila wiki siku ya jumanne

    ReplyDelete
  2. Mtangazaji bora wa taarifa ya habari

    ReplyDelete
  3. Miraji ni mtangazaji mwema na mwenye Sauti na ya kupendeza. Kipindi chake cha darubini kilinivutia Sana tangu utotoni.

    ReplyDelete
  4. Yukon wapi sasa jamani mchambuzi wa kisiasa wa kila wiki.aliwahi kuhusu dictator Paul pot sitasahau

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.