WAZIRI wa Nchi Afisi ya Makamu wa pili wa
Rais, Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed akizungumza na wananchi wa Tumbe Wilaya ya
Micheweni, ambao walikumbwa na maafa ya kuunguliwa nyumba zao moto hivi
karibuni, ambapo Waziri Aboud alikabidhi ubani wa shilingi milion tano na laki moja
kutoka kwa Rais wa Zanzibar dk Ali Mohamed Shein , kulia na mwakalishi wa
nafasi za wanawake Asha Bakar Makame (picha
na Haji Nassor, Pemba)
Nyumba zilizoungua moto hivi karibuni, huko
shehia ya Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, ambapo nyengine
zilibakia kuta na nyengine kusambaratika kabisa, (picha na Haji Nassor, Pemba )
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Makamu wa pili wa
Rais Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed, akimkabidhi Riziki Hamad Ali wa shehia ya
Madungu shilingi laki tano na nusu, za mkono wa pole kutoka kwa rais wa
Zanzibar dk Ali Mohamed Shein, ambapo Riziki ni mmoja tu kati ya wananchi
kadhaa Kisiwani Pemba, hivi karibuni waliokumbwa na maafa ya kuunguliwa nyumba
zao na moto uliodaiwa kuwa wa maajabu (picha
na Haji Nassor, Pemba)
No comments:
Post a Comment