Habari za Punde

Utingo alimwa faini 50,000 kwa kuning’inia

Na Husna Sheha

MAHAKAMA ya Wilaya Mfenesini imemtoza faini ya shilingi 50,000 utingo wa gari ya abiria wa njia namba 101 baada ya kukaa sehemu ya hatari ikiwa ikiwa kwenye mwendo.

Utingo huyo alitozwa faini hiyo baada ya kukubali kosa lake mbele ya hakimu Fatma Muhsin Omar baada ya kusomewa shitaka lake na mwendesha mashitaka, Khamis Abdurahman.

Kwa mujibu wa hati hiyo iliyowasilishwa mahakamani ilidaiwa kuwa utingo huyo wa gari yenye namba za usajili Z 484 CT ya njia namba 101 Mkokotoni,alipatikana ameakaa sehemu ya hatari kwenye kibao cha nyuma cha gari hiyo akiwa ananing'inia katika gari ikiwa katika mwendo.

Aidha hati hiyo ya mashitaka ilieleza kwamba kufanya kitendo hicho ni kinyume na kifungu cha 201 (1) sheria namba 7 ya mwaka 2003 sheria za usalama barabarani .

Upande huo wa mashitaka umefahamisha kuwa mshitakiwa huyo hana kumbu kumbu ya makosa ya nyuma. Hata hivyo mshitakiwa aliiomba mahakama imsamehe kwa vile ni kosa la mwanzo, lakini mahakama ilikataa na kumlima faini ya shilingo 50,000 au kutumikia chuo cha mafunzo mwezi mmoja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.