Coastal Union yanogewa na sukari Mtibwa
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KLABU ya Yanga, jana iliongeza kasi kuwafukuzia watani wao wa jadi Simba, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Hata hivyo, mabingwa hao wa Afrika Mashariki walilazimika kupigana kiume baada ya kutanguliwa kwa magoli mawili, ambapo hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza, Ruvu ilikuwa mbele kwa magoli 2-1.
Dakika mbili tu tangu kuanza kwa mchezo, nyavu za Yanga zilihujumiwa kwa bao la Seif Abdallah, kabla mchezaji huyo hajarudi kuifungia tena timu yake katika dakika ya tisa.
Kuona hivyo, Yanga ilianza kujipanga na kupeleka mashambulizi langoni mwa wageni wao, na katika dakika ya 20, Mbuyu Twite akacheka na nyavu baada ya kupiga mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja kimiani.
Mnamo dakika ya 35, Jeryson Tegete akaweka mambo sawa kwa kuiandikia Yanha bao la pili.
Baada ya hali kuwa sare, washambuliaji wa Yanga walihamia langoni mwa Ruvu Shooting, na kuiweka roho juu ngome ya timu hiyo hadi katika dakika ya 67, Didier Kavumbangu alipofanikiwa kuandika bao la ushindi.
Wakati hayo yakijiri Dar es Salaam, katika uwanja wa Mkwakwani Tanga, kocha Hemed Suleiman ‘Moroko’, alitoka na kicheko baada ya Coastal Union kuiadhibu Mtibwa Sugar kwa mabao 3-1.
Goli la kwanza la wagosi lilifungwa katika dakika ya 25, na Danny Lyanga akaongeza jengine kwenye dakika ya 38, na lile la tatu lilifungwa na Lameck Dyaton, huku Mtibwa ikifungiwa bao lake na Salum Sued mnamo dakika ya 40.
Simba itashuka katika uwanja wa Mkwakwani Tanga leo kuivaa Mgambo JKT.
No comments:
Post a Comment