Na Mwajuma Juma
TIMU ya Malindi iliyorudi ligi kuu ya Zanzibar kwa mbeleko ya mahakama, jana iliendelea kusakamwa baada ya kupigwa mabao 2-1 na Jamhuri katika uwanja wa Amaan.
Jamhuri ilianza kuzifumania nyavu katika dakika ya 21 kupitia kwa Abdallah Othman kabla Abdallah Abbas kuisawazishia Malindi kwenye dakika ya 33.
Baada ya mapumziko, Jamhuri iliongeza kasi na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Mbarouk Khamis kwa njia ya penelti katika dakika ya 68.
Malindi ingeweza kusawazisha katika dakika ya 55, lakini Amour Suleiman alipoteza mkwaju wa penelti.
Pamoja na kushinda, Jamhuri ilipata pigo baada ya mchezaji wake Mfaume Shaaban kufurushwa kwa kadi nyekundu kwa kitendo cha kumpiga Habib Hamad.
No comments:
Post a Comment