Habari za Punde

Ziara ya kujifunza kutembelea skuli za Maandalizi Stockholm

 Sehemu moja wapo ya ukumbi wa kuchezea watoto ndani ya skuli. Ukumbi huu hugeuzwa kila siku kutegemea mahitaji ya watoto. Watoto wakisema wanataka kucheza mchezo wa kujenga nyumba, kwa mfano, mazingira yanatengenezwa ya ujenzi wa nyumba. Ziara ya kutembelea skuli za maandalizi nchini Sweden inatoa changamoto ya haja ya kuleta Mageuzi makubwa katika ufundishaji wa watoto wadogo Makunduchi na pengine Zanzibar nzima
 Ndugu Mohamed Muombwa akionyeshwa miongoni mwa vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi wa Maandalizi kuanzia mwaka mmoja. Choo hiki kimepambwa baada wazee kuwataka walimu kukipamba choo hicho kwa njia itakayomfanya mtoto kuvutiwa. Jambo kubwa la kujifunza Kutoka skuli za maandalizi mjini Stockholm ni mashirikiano makubwa yaliyopo baina ya walimu Na wazee. Jambo nyengine ni kuwajengea watoto mazingira ya kupenda kuwa na hamu ya kujifunza
Wajumbe watatu wa wadi ya Makunduchi wamesharudi nyumbani kutoka Sweden lakini Mjumbe mmoja ndugu Mohamed Muombwa bado anaendelea na ziara mjini Stockholm kutembelea skuli za maandalizi. Elimu ya maandalizi Makunduchi bado iko nyuma, kwa hivyo wadi za Makunduchi zimekusudia kuleta mapinduzi katika eneo hilo ambalo ni muhimu mno kwa maendeleo ya elimu nchini. Picha inaonyesha ndugu Muombwa akiwa na mwalimu Mkuu Bi Lena Mattisson upande wa kulia na upande wa kushoto ni mwalimu Jennifer Andren Skulini Universum.
 
Picha zote kwa hisani ya Mohamed Muombwa ambaye yuko kwenye ziara maalum nchini Sweden

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.