Habari za Punde

Maziko ya Mchezaji wa Zamani waTimu ya Jeshi na Kikwajuni na Taifa ya Zanzibar Mohammed Shaa.

Jeneza lililokuwa na mwili wa Marehemu Mohammed Shaa Mohammed, ukitolewa katika msikiti wa Maisara baada ya kumaliza kuombewa dua na kusaliwa leo mchana kwa ajili ya kwenda kuzika Kijijini kwao Shakani wilaya ya Magharibi Unguja. Marehemu amefariki jana kwa kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria na kupelekwa katika hospitali ya Mnazi mmoja, 
Wananchi na wapenzi wa mchezo wa mpira wakiwa nje ya msikiti wa maisara wakisubiria kubeba jeneza la mwili wa marehemMohammed Shaa(PAPA SHA)

Wananchi wakiwa katika makaburi ya Shakani wakimzika marehemu Mohammed Shaa, aliefariki jana, kwa kuugua kwa muda mfupi baada ya kuugua homa ya maleria na kukimbizwa hospitali ya Mnazi Mmoja jana na kumkuta mauti katika hospitali hiyo.


Wananchi wakiomba dua baada ya kumaliza kuzika katika makaburi ya Shakani Unguja.

1 comment:

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.