Habari za Punde

Ziara ya Dk Shein Vietnam siku ya tatu

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Kamanda wa ulinzi katika kumbusho la Baba wa taifa la Vietnam, Ho Chi Minh,alipofika kutoa heshima akiwa ziarani nchini humo ya uhusiano na ushirikiano wa kukuza uchumi,baina pande mbili hizo
 Makamo wa Rais wa Vietnam Bibi Nguyen Thi Doan,(wa pili kushoto) na Viongozi wengine wa nchi hiyo wakiwa katika mkutano na Ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,ukiwa katika ziara ya kukuza uhusiano na ushirikiano katika nyanja mbali mbali za kukuza uchumi,Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Ikulu ya Nchi hiyo
  Rais wa Jamhuri ya Watu wa Vietnam Truong Tan Sang,akisalimiana na Ujumbe wa Maafisa na Viongozi waliofuatana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,Nchini humo katika kukuza mahusiano na ushirikiano katika pande mbili hizo

Rais wa Jamhuri ya Watu wa Vietnam Truong Tan Sang,akisalimiana na Ujumbe wa Maafisa na Viongozi waliofuatana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,Nchini humo katika kukuza mahusiano na ushirikiano katika pande mbili hizo.

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na Ujumbe aliofuatana nao walipofika katika kumbusho la Baba wa Taifa la nchini Vietnam,wakiwa katika gwaride maalum la uwekaji wa shada la mauwa katika kumbusho hilo liliopo katikati ya Mji wa Vietnam,alipokuwa katika ziara nchini huo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiweka shada la mauwa katika kumbusho la Baba wa Taifa la nchini Vietnam, liliopo katikati ya Mji wa Vietnam,ikiwa kama ishara ya kutoa heshima kwa kiongozi huyo,akiwa katika ziara nchini Vietnam
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifuatana na ujumbe aliofuatana nao baada ya kuweka shada la mauwa katika kumbusho la Baba wa Taifa la nchini Vietnam, liliopo katikati ya Mji wa Vietnam,kama ishara ya kutoa heshima kwa kiongozi huyo,akiwa katika ziara nchini Vietnam.

[Picha zote na Ramadhan Othman,Vietnam.]

2 comments:

  1. twashkuru sana ndugu yetu wajitahidi kutupasha matukio mbali mbali kila yanapojiri ila tatizo proofreading tu naona kidogo inakusumbua na jangine kurudiarudia maneno yale kwa yale imekuwa inatoa ladha la captionstory yote:
    ahsante

    ReplyDelete
  2. Sawa mdau tumekusoma. kweli proof reading ni tatizo sugu. Kujirudia maneno kwenye caption nadhani linakuja kutokana na picha zenye maelezo yanayolingana na hii ni kwa sababu ya kujaribu kuweka picha nyingi katika tukio moja. Na hili pia tutaliangalia. Shukran

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.