Habari za Punde

Tunahitaji kuendelezwa kitaaluma - Waratibu wa mradi wa ujasirimali Mkoa wa kusini Pemba

Na Zuwena Shaaban-Pemba 
                    
WARATIBU wa Mradi wa Ujasiriamali na Maisha kwa wanawake wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wamesema ipo haja ya kuendelezwa kitaaaluma kwa malengo ya kufanikisha azima zao mbali mbali zikiwemo zile za kuweza kugombea nafasi mbali mbali za uongozi.
Walisema pindipo watakuwa wakipata fursa za kuweza kuwezeshwa watakuwa ni wenye kupiga hatua kubwa katika kuendeleza na kupanga mikakati ya kufanikisha malengo hayo.
Hayo wameeleza wakati walipokuwa wakichangia mada ya ungozi kwa mwanamke na mada ya haki za binaadamu katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa weni Wilaya ya Wete.
Walisema jitihada za WEZA pekee ndio zilizowafikisha akinamama kuweza kutoka katika hali waliyokuwa nao na sasa akinamama hao kuweza kubadilika na kupata maendeleo .
Mmoja kati ya Waratibu hao Khadija Mohammed Said wa shehia ya Chwale alisema changamoto zipo nyingi katika jamii na hasa suala la kukosa elimu kwani ndio chanzo cha changamoto hizo.
Alifafanuwa kuwa jamii inataka kuweza kubadilishwa katika mambo yote ikiwa ni pamoja na kushawishiwa katika kufanya mambo ya meendeleo.
Naye Riziki Abdalla Kombo wa Shehia ya Mjananza Wilaya ya Wete alisema ingawa wajanajamii wanabadilika kidogo kidogo ila ipo haja ya kuwaelimisha ili nawa wao waweze kujitetea na kuweza kusimama na kugombea nafasi mbali mbali katika uongozi.
“Tunataka tugombee ila wanajamii wezetu wanaturudisha nyuma ila kupata semina hii imekuwa ni moja ya kuweza kujielewa na kuweza kujipanga na kusimama na tukaweza kugombea”alisema Riziki .
Walisema wataribu hao kuwa wamezidi kuelewa sifa na vipi mwanamke ambaye anahitaji kugombea katika nafasi mbali mbali moja ik,iwa ni kuweza kuwa na mashirikiano na wezake,awe ni mtu mwenye busara na mwenye kukubalika katika jamii.
“Mtu lazima awe muajibikaji ndipo atakapofanya kazi zake kwa uwajibaki bila ya kuweza kusimamiwa”walisema.
Aidha mshereheshaji katika semiana hiyo Hassan Abdalla Rashid kutoka Katiba na Sheria alisema mafunzo hayo yatawewezesha wanawake hao kujirtathmini na kuweza kujuwa ni vipi waweze kushiriki katika mambo mbali mbali ikiwemo la uongozi huku ikiwa ni watu wenye kujiaamini na kujuwa lipi wanalofanya.
Hata hivyo naye Afisa Uwezeshaji kutoka katika mradi wa ujasiriamali Pemba Jitihada Abdalla amesema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo wanawake katika kuelewa haki zao kwa upande wa kisiasa na kuweza kushiriki kugombea nafasi za uongozi katika kugombea .
Alisema katika harakati za kulilia ukombozi wa mwanamke umezidi kufanya kazi hususani katika suala la ufuatiliaji wa haki za binaadamu ik,iwa ni pamoja ya kuchagua na kuweza kuchagulia kwa mujibu wa sheria.
Semina hiyo ya siku tatu iliyofadhiliwa na shirika la umoja wa Mataifa linalosaidia maendeleo ya wanawake (UNWOMEN) liliwashirikisha Waratibu wa vikundi 30 kutoka katika shehia mbali mbali za Mkoa wa Kaskazini Pemba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.