Kesi ya inayowakabili viongozi
wakuu wa Jumuiya ya Uamsho iliyoendeshwa leo katika Mahakama kuu ya Vuga mjini Zanzibar
imebainisha kulikataa ombi la dhamana na kupelekea Viongozi hao kurudi tena
rumande.
Washtakiwa hao walifikishwa Mahkamani
hapo mnamo majira saa mbili na nusu asubuhi huku wakiwa chini ya ulinzi mkali
uliokuwa ukiongozwa na gari tatu za FFU pamoja na baadhi ya askari wa vikosi
vya KMKM.
Katika kesi hiyo, Jaji Mkusa Sepetu
amelazimika kulikataa ombi la dhamana kwa kudaiwa ya kwamba halikufuata taratibu
sahihi za kisheria, hivyo Mahakama imewataka Mawakili wa wateja hao kufuata
taratibu zilizo sahihi juu ya ombi lao la kupatiwa dhamana viongozi hao.
Kwa upande wa utetezi wa
washtakiwa hao kimsingi hawakufurahishwa na maamuzi yaliyoamuliwa na Mahakama
hiyo ya kulitupilia mbali ombi hilo la dhamana kwani wamesema hoja iliyotolewa
uamuzi si miongoni mwa hoja iliowasilishwa kwa DPP
Kimsingi wamesema ni hoja iliyoibuliwa
na Mahakama wenyewe jambo ambalo linawapa mashaka mawakili hao.
Aidha wamesema kuwa wallipanga
kuwasilisha ombi jipya leo hii la kudai dhamana kwa wateja wao lakini kutokana
na muda kutokuruhusu kwa siku ya leo wameamuwa kujipanga upya zaidi na
kuwasilisha maombi hayo hapo kesho.
Kesi hio itasikilizwa tena mnamo
tarehe 3/1/2013
No comments:
Post a Comment