Mshindi wa tatu Epiq BSS-Wababa Mtuka
Wababa, ambaye alitoa ushindani mkali
kwa Walter na Salma, amesema anaamini wimbo huo utakuwa mkali na utashika sana
wapenda burudani hapa nchini.
‘Nimetoa wimbo huu kama zawadi ya
sikukuu kwa mashabiki wangu wote ambao wamenisapoti kipindi chote cha
mashindano, lakini pia shukrani za pekee ziende kwa Zantel kwa kunirekodia
wimbo huu’ alisema Wababa.
Wimbo huo, ambao ndio wa kwanza
kutambulishwa kati ya nyimbo zote za washiriki wa Epiq BSS, umedhaminiwa na
kampuni ya Zantel kama ahadi yake ya kuwarekodia bure wasanii waliongia 12 bora
ya Epiq BSS.
Nyimbo nyingine za washiriki wa Epiq
BSS zitaachiwa mwishoni mwa wiki hii.
No comments:
Post a Comment