Spika
wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho amesema zowezi linaoendelea la ukusanyaji wa maoni kuhusiana na Katiba Mpya
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
linalenga kupata Muungano mzuri zaidi
utakaomaliza malalamiko ya pande
zote za Muungano huo.
Spika Kificho amesema hayo leo wakati
akizungumza na Balozi wa Canada hapa nchini Bw. Alexandre Leveque huko Ofisini kwake Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Amesema zowezi hilo linaendelea vizuri ambapo wananchi na makundi mbali mbali yanaendelea kutoa maoni yao kuhusiana na Katiba Mpya pamoja na mwelekeo wa Muunndo wa Muungano
wanautarajia ambao wanahisi utaleta
maslahi zaidi kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
Amesema Muungano wa Tanzania ni wa pekee ambao
unahitaji kutunzwa na kuendelezwa ingawa wananchi wamekuwa na mawazo tofauti
juu ya mfumo wanaouhitaji .
Mhe Kificho amesema katika kuudumisha Muungano huo ni vyema kuyapatia ufumbuzi malalamiko ya kila upande ikiwa ni pamoja na kufahamika vyema mambo ya
muungano na yale yasiyokuwa ya Muungano.
Amefahamisha kwamba zowezi la
uchukuaji wa maoni ni muhimu kwa
wananchi na kutokana na umuhimu huo
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar chini ya ufadhili wa Serikali ya Norway limechukua
juhudi ya kutoa elimu ya katiba pamoja na kutayarisha kitabu maalum cha
Elimu ya Katiba ili kuwapamwangaza
wananchi hao kuhusiana na Katiba yao.
Kwa
upande wake Balozi Alexandre Leveque amesema mpango wa kukusanya maoni ya wananchi wakati
wa kuunda katiba ni jambo zuri lenye kuonyesha kukomaa kwa demokrasia hapa
nchini.
Amesema nchi yake inatarajia kuona Watanzania
wanapata katiba yenye mafanikio ambapo Canada itafuatilia kwa karibu mwenendo
wa mchakato wa Upatikanaji wa katiba mpya na nchi hiyo itatoa kila aina ya
ushirikiano ili kuhakikisha kwamba
zowezi hilo linafanikiwa.
Uzuri wa Muungano na ubaya wa Muungano wanaujuwa Wananchi wenyewe, ikiwa Upande moja unahisi hauna benefit kwao Basi viongozi wanyamaze kimya wananchi ndio sauti ya mwicho sio kuonekana mbumbubu wasio fahamu shida na raha.
ReplyDeleteKificho yeye ni mtumichi tu wa wananchi sio Master wa kuwa lazimisha Muungano.
Kwake una Benefit alikwisha zitaja kuwa kaekeza vitega uchumi Tanganyika na kuwa na majumba , ndio akaulazimisha uweko kwa Maslahi yake sio ya wazanzibar walio wengi ndani ya Zanzibar yenyewe.
wewe mwandishi hii nchi yetu inaitwa zanzibar wala sio tanzania zanzibar. kificho wewe unafaidika lakini raia wa kawaida wanateseka. ukifika wakati wa kuamua watatoa msimamo wao kuhusu nchi yao.
ReplyDeleteKwa anaeijua Zanzibar inavyoendeshwa, hawezi kusema kua inaonewa bali atasema kua inajionea au tunajionea wenyewe.
ReplyDeleteMtu yeyote naesema Zanzibar inaonewa aidha ni mgeni hapa au anajipumbaza.
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeletesasa unategemea nini kutoka kwa kificho mtu mwenye elimu ya kuunga
ReplyDelete