Habari za Punde

Ziara ya Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali Zanzibar Ofisi za E-Gorvement Mazizini

Mkurugenzi wa Idara ya Vitambulisho Zanzibar na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Mkonge wa Mawasiliano Zanzibar akitowa maelezo kwa waandishi wa Habari waVyombo mbalimali Vilioko Zanzibar.
Waandishi wa habari wakitembelea Ofisi za Mkonge wa Mawasiliano Zanzibar kujionea huduma za Mawasiliano zitakazopatikana kupitia mkonge huo katika Visiwa vya Unguja na Pemba.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Mkonge wa Mawasiliano akiwaonesha waandishi maeneo michoro ya sehemu ilioungwa kwa kutowa huduma hiyo, yalioungwa kupitia mkonge huwa kwa baadhi ya Ofisi ambazo tayari zimekamilisha huduma zake.

Waandishi wakitembelea Kituo cha Mawasiliano.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Mkonge wa Mawasiliano akiwaonyesha waandishi Waya wa Faiba ambao unatowa huduma ya mawasiliano katika nkwenge huo wakati wa ziara yao kutembelea Ofisi hiyo kujionea jinsi ya ufanisi wa Mawasiliano kupitia katika waya huo wa faiba.

1 comment:

  1. Je hizo huduma za e-government zishaanza au ndo wenzetu wafanye nasi tuige bila ya kuwa na mipangilio ? Wizara ngapi zishaunganishwa ? Skuli na mahospitali je ? Tuliambiwa Zan ID zitakuwa suluhisho la wafanyakazi hewa ,je ni hivyo ? Kama laa kwa sababu gani ? Au kuna watu ndo wana mradi huo wa wafanyakazi hewa ? Hili ni tatizo dogo tu kama kutakuwa na uwazi...kila mfanyakazi wa SMZ alipwe kutumia benki PBZ, hii itasaidia hiyo benki na pia kukata hii fitna ya kuibiana kila uchao.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.