Habari za Punde

Dk Shein ahitimisha ziara yake Mkoa wa Kaskazini Pemba

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) akizungumza na viongozi wa Kampuni ya LEA Associates South Asia Pvt.Ltd,chini ya ufadhili wa
shirika la MCC la Marekani,inayojenga Barabara ya  Bahanasa,Dayan na Makongeni  Mkoa wa Kaskazini Pemba, alipokuwa katika ziara ya kutembelea miradi mbali mbali ndani ya Mkoa huo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na wafanyakazi wa kampuni ya LEA Associates South AsiaPvt.Ltd,chini ya ufadhili wa shirika la MCC la Marekani, inayojenga barabara ya  Barabara ya Bahanasa , Dayan na Makongeni, akiwa katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kaskazini Pemba
 Msaidizi wa Mhandisi wa Ujenzi wa Mradi wa ujenzi wa Barabara Kampuni ya Mecco yenye makao Makuu yake Dar es Salaam,Suleiman Iddi,akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) alipotembelea barabara ya Gando- Konde jana,akiwa katika ziara ya Mkoa huo
 Mkaazi wa Jimbo la Gando,Khamis Ali Khamis,akitoa malalamiko yake kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kuhusu malipo ya nyumba zilizoathirika katika ujenzi wa Barabara ya Wete-Konde,inayojengwa na kampuni ya Mecco,alipofika Rais jana akiwa katika Ziara ya Mkoa wa Kaskazini Pemba kutembelea maendeleo ya Miradi ya ujenzi wa Barabara hiyo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Viongozi mbali mbali naWatendaji wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, katika Mkutano wa Majumuisho ya ziara yake iliyomalizika jana katika Mkoa huo, mkutano ilifanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba
Baadhi ya Watendaji wa Ofisi mbali mbali za Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na watendaji hao katika Mkutano wa Majumuisho ya ziara yake iliyoifanya ndani ya Mkoa huo,mkutano ilifanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba.
 
[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.