Habari za Punde

Utiaji Saini za Mikataba ya ushirikian​o kati ya Tanzania na China

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais wa China Xi Jinping,jana Ikulu Jijini Dar es Salaam,wakati wa utiajisaini makubaliano ya mashirikiano ya kukuza masuala ya kiuchumi na kijamii katika ukumbi wa mikutano Ikulu,(katikati) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete
 Rais wa China Xi Jinping,(kushoto) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,(katikati) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kushoto) pamoja na viongozi watakao tia saini mikataba mbali mbali ya makubaliano kati ya Serikali ya China na Tanzania Ikulu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo,Omar Yussuf Mzee,(kulia)akitiliana saini na Waziri wa Biashara wa China, Bw.Gao Hucheng,makubaliano ya ushirikiano kuhusu vifaa vya Hospitali ya Abdalla Mzee na Vifaa vya uchunguzi wa makontena katika Bandari ya malindi Zanzibar,saini ya makubaliano ilitiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam jana,Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakishuhudia
  Rais wa China Xi Jinping,(wa tatu kushoto) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,(wa pili kushoto) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein,(kushoto) pamoja na viongozi wa Serikali ya China, watakao tia saini mikataba mbali mbali ya makubaliano na Serikali ya Tanzania Ikulu
 Waziri wa Fedha wa Tanzania Dr.Willium Mgimwa, akibadilishana mikataba katika Nyanja za ushirikiano wa kitaalmu na kiuchumi na waziri wa Biashara wa China Bw,Gao Hucheng,baada ya kutialiana saini makubaliano hayo ikulu Jijini Dar Salaam
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na Mke wa Rais wa China Peng Liyuan,pamoja na viongozi wa ujumbe Serikali ya Jamhuri watu wa China na Tanzania akiwa katika chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Rais Dk.Jakaya Kikwete,Ikulu Jijini Dar es Salaam

Picha zote na Ramadhan Othman, Dar es Salaam

2 comments:

  1. msidanganywe waznz , mikataba yote muhimu watasaini na kuchukuwa watngnk , hio yote ni kuonyesha kama vile kuna usawa fulani ktk muungano, hatuutaki muungano wowote uleeeeeeeeee , hata mkijidai kutudanganya kwa peremende

    ReplyDelete
  2. Huu upo tu, mkataka msitake!..kama mna hoja za msingi juu ya namna bora ya kuisukuma mbele Z'bar kimaendeleo leteni lakni kwa hili mnapoteza mda bure!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.