Habari za Punde

Uzinduzi wa Usajili wa Ardhi Viwanja vya Bustani ya Victoria










RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mrajis wa Ardhi Mwanamkaa A Mohammed, akilelezea maeneo yaliofanyiwa usajili wa ardhi katika zoezi hilo la usajili kwa Wananchi wa Mji Mkongwe na maeneo mengine ya Unguja wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya bustani ya Victoria.kulia Balozi wa Filand nchini Tanzania Sinikka Antila,na kushoto Waziri wa Ardhi Abdalla Ramadhani Shaban
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akihutubia katika uzinduzi wa Usajili ya Ardhi katika viwanja vya bustani ya Victoria vuga.    



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akihutubia katika uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya bustani ya Victoria Vuga.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa Hati ya Ardhi namba moja ya eneo la Ikulu Zanzibar na Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nisharti Abdalla Ramadhani Shaban, na kulia Balozi wa Filand  Sinikka Anitala, wakiangalia hati hiyo na kupata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ardhi.




RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Hati yake ya Usajili wa Ardhi mkaazi wa Vuga Maryam Hadhir Mohammed,wakati wa uzinduzi huo.uliofanyika katika viwanja vya bustani ya Victoria.


BALOZI wa Filand Tanzania Sinikka Anitala, akimkabidhi zawadi ya Picha za Visiwa vya Unguja na Pemba ambavyo vimefanyiwa zoezi ya usajili wa ardhi wa maeneo hayo wakati wa uzinduzi wa Usajili wa Ardhi Zanzibar katika viwanja vua bustani ya Victoria




WANANCHI waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa usajili wa ardhi Zanzibar katika viwanja vya bustani ya Victoria wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika hafla hiyo.










3 comments:

  1. Kaka hapa umetuacha njia panda, picha nyingi hazina maelezo.

    Kama kuna jambo ambalo watu wengi hapa wanahitaji kulijua basi ni usajili wa ardhi kwa hivyo kama kuna makala inayofafanua zaidi usiache kutuwekea.

    ReplyDelete
  2. Ahsante ndugu Othman kwa habari za picha zako. Natumai unatembelea maoni na kusoma maoni yetu.. Kazi unayofanya ni nzuri sana lakini nimekua nikiona makala zako au picha zako zinarudia maneno hayop hayo kila wakati baada yakupata habari nyengine zinazoendana na picha....

    kama mifano hiyo ya picha zako imekua inajirudia kila wakati maelezo hayo hayop kila picha... Mfano " badala yakufupisha nakueleza hasa madhumuni ya picha badala yakueleza majina na maelozo hayo hayo...

    ReplyDelete
  3. Sasa hizi hati zinatolewa kwa wasta au? Manake kuna wengine tumepeleka nyaraka zote tangu 2008 mpaka sasa wanazingua watu.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.