Na Masanja Mabula -Pemba
Mbunge wa Jimbo la Konde Khatib Said Vijana hapa nchini wametakiwa kutambua kuwa sekta ya michezo ni sehemu ambayo inayoweza kuzalisha ajira na kuwasisitiza kushughulikia michezo ikiwemo ni sehemu ya kujipatia kipato .
Akizungumza na wajumbe wa kamati ya kusimamia mashindano ya kuwania kombe la Mbunge pamoja na viongozi wa vilabu , Khatib amesema kuwa tatizo la ajira linaweza kupungua ikiwa vijana watatambua umuhimu wa Sekta hiyo katika kupungua tatizo hilo .
" Naomba mtambue ya kwamba michezo ni moja ya sekta ambazo zimekuwa sikiisaidia sana Serikali katika kupunguza tatizo la Ajira kwani kupitia sekta hiyo vijana wengi wameajiriwa na kipato chao kinaridhisha " alifahamisha .
Aidha Mbunge huyo ameitumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa timu kusimamia vyema suala la nidhamu kwa wachezaji na mashabiki wa timu zao , ili kuweza kuzalisha wachezaji wenye nidhamu ndani na nje ya uwanja .
Wakichangia katika kikao hicho baadhi ya viongozi wa vilabu waliitaka kamati ya mashindano hayo kuwa makini na suala la waamuzi na kuitaka kutosita kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria waamuzi wakaozibeba baadhi ya timu .
Walisema kuwa ni vyema kamati hiyo ikawapiga msasa waamuzi watakaochezesha michuano hiyo kabla ya kuanza kwa ngarambe hizo . .
Kwa mujibu wa Mbunge huyo ni kwamba mshindi wa kwanza katika mashindano hayo ityazawadiwa shilingi milioni moja , wa pili 650,000/ wakati mshindi wa tatu atajizolea shilingi 250,0000 .
Taarifa zaidi zinasema kuwa kila timu ambayo itashiriki katika mshindano hayo itapatiwa mipira mitano pamoja na seti moja ya jezi ikiwa ni vifaa kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ambapo zaidi ya timu 20 zinatarajia kushiriki
No comments:
Post a Comment