Habari za Punde

‘Zanzibar iwekeze utalii wa gofu’

Na Mwantanga Ame
 
KAMISHENI ya Utalii Zanzibar, imeshauriwakuangalia uwezekano wa kutafuta wawekezaji watakaoweza kuanzisha utalii kupitia mchezo wa gofu.
 
Ushauri huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mbele ya viongozi wa Kamisheni hiyo, alipokuwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, mjini Zanzibar.
 
Balozi Seif, alisema ipo haja kungalia namna ya kuwekeza katika utalii wa mchezo huo, ambao uliipatia sifa sana Zanzibar miaka ya nyuma, ingawa kwa sasa unaonekana kusahaulika.


Alieleza kuwa, baadhi ya mataifa duniani, yamepata mafanikio makubwa kiuchumi kutokana na kutumia utalii wa gofu, hivyo ni vyema Zanzibar iufanyie kazi ushauri huo.
 
Ili kufanikisha azma hiyo, alisema ni vyema wizara inayoshughulikia michezo na utalii, katika mikakati yake ya miradi ya maendeleo, iandae mpango wa kumiliki angalau uwanja mmoja wa mchezo huo, wakati serikali ikiendelea na jitihada za kutafuta wawekezaji katika eneo hilo .#
 
“Inasikitisha kuona michezo mingi ya ndani iliyoiletea sifa Zanzibar ikiwemo gofu, hoki, riadha na mpira wa miguu, ama imekufa au inasuasua”, alifahamisha.
 
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Issa Mlingoti Ali, aliahidi kuufanyia kazi ushauri wa Balozi Seif, na kukumbusha kuwa, serikali kupitia taasisi ya Uwekezaji Vitega Uchumi iliwahi kupokea maombi ya wawekezaji watatu waliokuwa na nia ya kujenga viwanja vya gofu, lakini haifahamiki mpango huo ulikoishia.

3 comments:

  1. Sioni cha kusoma zaidi ya kichwa cha khabari kunani?

    ReplyDelete
  2. Kaka turekebishie..hakionekani kitu.
    Ahsante

    ReplyDelete
  3. Mkiambiwa msimamie vizuri ardhi chache tuliyonayo, mnaona kama vile mnafundishwa utawala. haya sasa tuone wapi mtatoa eneo la kujenga kiwanja cha gofu manake baadhi ya wahadimu wanadhani kiwanja cha Gofu ni kama kile cha mpira(mia 100)!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.