Habari za Punde

Jumuiya ya Uvuvi na mazingira endelevu Zanzibar yachagua viongozi

 Mmoja ya wanachama wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar Haji Khamis Hasan, akipiga kura kuwachaguwa viongozi mbalimbali watakayo iyongoza Jumuiya hiyo
 Katibu wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar Husen Muhammed Makame, akionyosha Cheti cha usajili pamoja na Katiba ya Jumuiya hiyo huko katika Skuli ya Sekondari ya JKU Mtoni.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar Sheha Chum Mngana, akizungumza na wanachama mara tu baada ya kumaliza kwa uchaguzi huko katika Skuli ya Sekondari ya JKU Mtoni.
Picha ya pamoja ya wanachama wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar baada ya kumalizika kwa uchaguzi uliowachagua viongozi mbalimbali wa Jumuiya hiyo.(PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO ZANZIBAR.)
 
Miza Othman Maelezo    
 
Imelezwa kuwa iwapo patakua na mashirikiano katika Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar (ZFSE) iliyopo Mtoni Kidatu hakuna sababu ya umoja huo kutoyafikia malengo waliyojipangia.

Hayo yamelezwa na Mwenyekiti wa ZFSE Sheha Chumu Mngana wakati alipokuwa akizungumza na wanjumuiya hiyo baada ya kuchaguliwa rasmi kuongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu katika uchaguzi uliofanyika skuli ya sekondari ya JKU Mtoni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Amesema ni vyema kwa Jumuiya hiyo kutekeleza majumu yao waliojipangia pamoja na kubuni miradi mbali mbali ili kuleta maendeleo katika Jumuiya yao.

‘’Bila mashirikiano, hatutofikia popote, kuwa makini au kujielewa na kutekeleza majukumu na kila mwanachama anawajibu wa kupatiwa haki’’ Alisema Sheha Chumu Mngana.



Katika uchaguzi huo wamechaguliwa wajumbe wanne wa Kamati Kuu ikiwa ni njia mojawapo ya kuipa nguvu jumuiya hiyo ambao ni Zena Husein Suwedi, Haji Khamis Hassan, Mansab Ramadhan Mansab na Mashavu Mzee Moh’d.

Aidha Mwenyekiti Sheha Chumu amesema Jumuiya yao yenye wanachama 20 wakiwemo wanaume 10 na wanawake 10 inakabiliwa na changamoto mbali mbali katika ikiwemo ofisi ya kudumu pamoja na vitendea kazi jambo ambalo linapelekea kukwamisha ufanisi wa Jumuiya yao.

Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar ilianzishwa mwaka jana na imepatiwa usajili rasmi tarehe 12 /4/ 2013 na Mrajisi Mkuu wa Serikali Nd. Abdallah Wazir.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.