Habari za Punde

Kamishna Mussa:Waliokamatwa na Silaha ni wahusika wakuu wa matukio ya kijambazi Z'bar

UCHUNGUZI WA KISAYANSI UMEFANIKISHA KUKAMATA SMG NA RISASI 29, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa akionesha Bunduki aina ya SMG katika mkutano na waandishi wa habari, ambayo imekamatwa kwa mfanyabiashara wa dhahabu Mohamed Ali Salum, dukani kwake Mkunazini, karibu na msikiti wa Jibril, mjini Zanzibar.

Jeshi la Polisi Zanzibar limefanikiwa kuwakamata watu wawili ambao wanasadikiwa kuwa majambazi,waliokamatwa wakiwa na silaha ya SMG yenye risasi 29 ndani yake.


Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake makao makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar ziwani,Kamishna Mussa Ali Musaa aliwataja watu hao ambao ni Faustine Geogre miaka 36 Msukuma wa geita Ushirombo na Mohamed Ali Salum wa Bambuu, Bububu.
 
PhotoAlisema kuwa awali Jeshi lake lilifanikiwa kumkamata Faustine wakati akiwa kwenye sehemu za starehe (baa ya chuo cha mafunzo)ambae walimfanyia mahojiano na badae kumpekuwa na kumkuta akiwa na fedha za kigeni Dola za kimarekani 100, Naira za Nigeria 3540 na T,shs,370,000/= pamoja na simu 3 aina mbali mbali.

                                                       
 

Kutokana na hatua hiyo ndipo Jeshi hilo badae likaamua kufanya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kumkuta na vitu vyengine kadhaa vikiwemo jeki 1, bisbisi 2, koleo la kukatia nyaya na baadhi ya vitu vyengine kadhaa alisema kamishna Mussa.

Aidha kamishna huyo alifahamisha kuwa kutokana na kumuhoji mtuhumiwa huyo kuhusu Bunduki anayotumia katika shughuli zake za ujambazi alisema kuwa bunduki anayotumia na baadhi ya vitu vyengine vilivoibiwa viko nyumbani kwa Mohamed Ali Salum wa Bububu ndipo jeshi hilo likaweza kumkamata mtuhumiwa huyo mnamo tarehe 12/4/2013 saa nne usiku akiwa nyumbani kwake Bububu.


Ndipo Jeshi hilo kama kawaida yake lilifanya upekuzi nyumbani kwa kijana huyo na kukuta simu 1 samsung touch na ipad ndogo nyeupe na baadae kufanya upekuzi mwengine dukani kwake mkunazini na kufanikiwa kukuta Bunduki SMG iliyokatwa kitako yenye nambari 56-375085 ambayo ilikuwa na risasi 29 ambayo imefanyiwa matengenezo ili iwezi kupiga risasi moja moja.

Akibainisha baadhi ya vitu vyengine ambavo vimekutwa ndani ya duka kuwa ni kamishna amesema kuwa ni glove pia moja soksi za kuvalia kichwani nyeusi na kisu kikubwa,pamoja na vitu kadhaa vikiwemo laptop na baadhi ya vitu vyengine ambavyo vikasadikiwa kuwa vimeibiwa.

Sambamba na hayo kamishna Mussa amesema kuwa Jeshi lake litaendelea na Operesheni ya namna hii za kuwasaka wahalifu kama kawaida ili kuhakikisha uhalisu unatoweka nchini kwetu,pia ametowa wito kwa wananchi wote waendelee kutoa taarifa kwa Jeshi hilo ili kukomeza uhalifu unaondelea siku hadi siku

1 comment:

  1. hiindiyo kazi ya polisi kukamtawahalifu tushachokanamatokeohaya,kamanda, musa,isiwehaotu,msakouendelee, mpakavibaka wadogo wanaosumbua mitaani

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.