Habari za Punde

Makamu wa Rais Dkt Bilal Aendesha Harambee ya Mfuko wa Udhamini Elimu ya Juu wa MWALIMU NYERERE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika jana Aprili 8, 2013 katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam. Katika Harambee hiyo zilikusanywa fedha taslimu  shilingi milioni 71 na ahadi ya fedha za Kitanzania shilingi milioni 658.

 Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha moja ya Sarafu iliyopigwa mnada katika harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika jana Aprili 8, 2013 katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam, ambayo ilinunuliwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi kwa Sh. milioni 20. Kushoto ni Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa. Harambee hiyo ilifanyika jana. katika Ukumbi wa BOT
 Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi sarafu Dkt. Charles  Kimei, baada ya kuinunua sarafu hiyo kwa Sh. milioni 19 katika mnada wa Harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika jana April 8, 2013 katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa harambee hiyo. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.