Habari za Punde

Maziko ya mdogo wake Dk Bilal , Haji Gharib Bilal yafanyika leo


Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,akiongoza Swala ya maiti ya Marehemu Haji Gharib Bilali, Mdogo wake Makamo wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal,katika msikiti wa Kilimani Mjini Zanzibar,ambapo viongozi mbali
mbali wa Kitaifa walihudhuria katika msiba huo, na kuzikwa Mwera,Wilaya ya Magharibi Unguja



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,,akitia udongo katika kaburi la Marehemu Haji Gharib Bilali, Mdogo wake Makamo wa Rais wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal, wakati wa maziko yaliyofanyika leo jioni huko Mwera,Wilaya ya Magharibi Unguja

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,akitia udongo katika kaburi la Marehemu Haji Gharib Bilali, Mdogo wake Makamo wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal, wakati wa maziko yaliyofanyika leo jioni huko Mwera,Wilaya ya Magharibi Unguja

4 comments:

  1. Maraisi wetu walipolaumiwa kwa kutohudhuria baadhi ya mazishi ya mashekhe mashuhuri hapa nchini lakini wanahudhuria mazishi ya mapadri walidai kwamba kwa waislamu muda huwa hautoshi kuandaa safari ya raisi tofauti na wakristo ambao maiti huwekwa kwa muda, cha ajabu mazishi haya wamepatikana wote tena kwa muda huo mfupi jee kulikoni waislamu wanapotoa hoja zao musizipuuze viongozi wetu.

    Tunamuombea ALLAH ailaze roho ya Marehemu mahal a pema peponi, aamiina.

    ReplyDelete
  2. kwa kutohudhuria mazishi ya Sheikh wetu Mar Nassor Bachu viongozi wa Serikali sio sababu kuwa sheikh wetu hatokwenda peponi. Inshallah ALLAH atampa Pepo ya juu kabisa FIRDAUS Ameen.

    ReplyDelete
  3. Safari yake iwe ya kheri inshaallah,ampe malazi mema peponi yeye na umma wote wa Muhammad(S.W.A)Amee.

    ReplyDelete
  4. Pumzika kwa amani mjomba umeteseka kwa muda mrefu, Mungu atupe imani ya kuendelea kukuombea dua kama vitabu vya dini vinavyosema.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.