Habari za Punde

Uvumi kwamba Rais Mstaafu Aboud Jumbe kwamba amefariki siyo kweli

Kuna uvumi uliovuma kwa nguvu leo hii katika visiwa vya Zanzibar kwamba aliekuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Aboud Jumbe Mwinyi naye amefariki dunia asubuhi hii ya leo.
 
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika tulizozipata ni kwamba mzee wetu, Mhe Aboud Jumbe ni mzima na yupo nyumbani kwake Mji mwema Kigamboni , Dar es Salaam anaendelea na shughuli zake kama kawaida.
 
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.