Habari za Punde

Maziko ya Msanii Mkongwe Zanzibar Bi Kidude

NAIBU Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Bi.Hindi Hamad, akijumuika na Wananchi katika mazishi ya Msanii maaruf Zanzibar Bi Kidude yaliofanyika nyumbani kwake Rahaleo.
WANANCHI wakihudhuria katika mazishi ya Msanii Maarufu Zanzibar Fatma Binti Baraka Bi.Kidude, yaliofanyika nyumbani kwake Rahaleo wakisoma hitma kabla ya kutoka mwili wa marehemu kwenda kuzikwa kijiji kwake Kitumba nje ya Mji wa Zanzibar jana.

MSANII wa Muziki wa DiscoDJ BHAA, Mwakilishi wa Jimbola Bububu Hussein Ibrahim Makungu,(BHAA) akiwa na wananchi wakiwa wamebeba jeneza la marehemu Bi Kidude wakiingia katika Masjid Mushawar Muembeshauri kwa ajili ya kuusalima mwili huo jana.
MSANII wa Muziki wa Bongo Flava Diamond wakiingikla katika viwanja vya Masjid Mushawar muembeshauri kujumuika na Wananchi katika mazishi ya Msanii Mkonwe wa Zanzibar Bi Kidude, aliyefariki juzi.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakisoma hitma ya marehemu Bi Kidude katika Masjid Mushawar Muembeshauri.
Wananchi waliohudhuria maziko ya Bi Kidude wakiwa nje ya Masjad Mushawar, wakisubiri kutoka kwa Jeneza kwenda kuzika katika makaburi ya Kitumba.
Waumini wa Dini ya Kiislam wakiuombea dua mwili wa marenemu Bi Kidude baada ya kuusalia katika Masjid Mushawar Muembeshauri.iliosomwa na Shekh Ali Anni  
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Khamis Haji Khamis. akiomba dua baada ya kumaliza Sala ya kuuombea mwili wa marehemu Bi Kidude . 





Mvua iliyokuwa ikinyesha kwa nguvu haikuwazuia  watu wengi waliofika shamba Kitumba kwenye maziko ya Bi Kidude

Rais wa jamhuri ya Muungao Dk Jakaya Kikwete akifuatiwa na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein walipofika Kitumba yalipofanyika maziko ya Bi Kidude

Umati wa waumini waliohudhuria maziko ya Bi kidude wakitanguliza jeneza la Bi Kidude tayari kwa safari yake kupelekwa Kitumba kwa mazishi
Mwili wa Bi Kidude ukitolewa kutoka kwenye jeneza kwa ajili ya kuhifadhiwa katika kaburi
 Vijana waliobeba Jeneza la mwili wa Marehemu Msanii maarufu Fatma Binti Baraka (kidude) wakati wa maziko yake yaliyofanyika leo huko kijijini kwao Kitumba,Wilaya ya Kati Unguja, ambapo maziko yake yamehudhuriwa na wasanii mbali mbali ndani na nje ya nchi.
 Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika maziko ya marehemu Bi Fatma Baraka (Kidude) kijijini kwao Kitumba,Wilaya ya Katr Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(kutoka kulia) Rais wa jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif,na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,wakiitikia dua baada ya maziko ya Msanii maarufu Fatma Binti Baraka (kidude) aliyefariki jana na kuzikwa leo Kijijini kwao Kitumba,Wilaya ya Katri Unguja.

1 comment:

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.