Habari za Punde

PBZ Islamic Bank na PBZ zatowa misaada kwa Madrasa na Skuli Zanzibar.

 Meneja Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Seif Suleiman, akimkabidhi mifuko ya saruji 80 Mwalimu Mohammed Juma,  wa Madrasa Al Hayriya Islamic ya Mpendae, kwa ajili ya kujengea jengo la Madrasa hiyo, iliotolewa na PBZ Islamic Bank, ikiwa ni moja ya faida zake inaopata kwa wateja wake wanaotumia PBZ Islam Bank  na kutumia kwa kutowa misaada katika Jamii.   
 Meneja Masoko ea Benki wa Watu wa Zanzibar Seif Suleiman kushoto akimkabidhi msaada wa Mabati 30 na Saruji 28, Mwalim Simai Mohammed kwa ajili ya ujenzi wa Vyoo katika ya Skuli ya Tumbatu. Msaada huo umetolewa na Benki ya Watu wa Zanzibar kwa ajili ya kusaidia Jamii katika shughuli za maendeleo, ikiwa ni kutumia faida yake inayoipata kutowa misaada hiyo kwa Wananchi na kuendeleza mahusiano na wateja wao  pamoja na kuitangaza PBZ kwa Wananchi na kujuwa shughuli zake inazozifanya.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.