Habari za Punde

Utaratibu wa Maziko ya Bikidude Yatafanyika Nyumbani kwake Rahaleo Kesho.

 Gari ikiwa na Mwili wa marehemu Bi Kidude ukiusafirisha kutoka katika Kijiji cha Kihinani kuupeleka nyumbani kwake Rahaleo kwa matayarisho ya mazishi kesho mchana na kuzikwa Kitumba. Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
 Mwili wa marehemu ukishushwa katika gari wakat ukiwasili nyumbani kwake Rahaleo kwa taratibu za mazishi kesho mchana na kuzikwa Kitumba.
Ndugu na Jamaa wakiubeba mwili wa marehemu BiKidude wakati ulipowasili nyumbani kwake Rahaleo kwa ajili ya mazishi  kesho.
Mrajisi wa Baraza la Sanaa Zanzibar Khadija Batashi akizungumza na Waandishi jinsi alivyoupokea msiba wa Bi Kikdude
 Matayarishi ya mazishi ya Bi Kidude yakitayarishwa katika Nyumba yake Rahaleo.
 Mjuukuu wa Bi Kidude Omar Ameir akiwasiliana na jamaa kuwajulisha msiba wa Marehemu Bi. Kidude, baada ya kuwasili katika nyumba yake kwa matayarisho ya mazishi kesho mchana saa saba baada ya sala ya adhuhuri na kuzikwa Kitumba.   
 Bi.Maryam Hamdani akilakiwa na Bi Sihaba baada ya kuwasili katika makazi ya bikidude rahaleo , akiwa na majonzi.  
 Waandishi wa habari wakizungumza na Mfadhili Mkubwa wa Bi Kidude Maryam Hamdan,kuhusiana na marehemu ambaye yeye alikuwa ni mtayarishaji na mratibu wa safari za Bi Kidude nje ya Nchi katika matamasha mbalimbali aliyokuwa akihudhuria nje ya nchi katika uhai wake.
Meneja wa Sauti ya BUSARA Zanzibar Stella Steven, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na marehemu Bi Kidude ambaye alikuwa akidhaminiwa na BUSARA katika matamasha mbalimbaliyaliokuwa yakiandaliwa na Busara.jinsi walivyopokea kifo chake kwa masikitiko makubwa na kuacha pengo katika tasnia ya muziki wa taarab asilia Zanzibar. 

3 comments:

  1. mungu amlazemahalapema,kwanikilanapsi,itaonjamauti,inatakiwa tuuenzi,kazinajuhudiyakektk kuitangaza,zanzibar


    ReplyDelete
  2. bikidude,kafajekazzizakepiazitakufa

    ReplyDelete
  3. Aibu na imasikitisha sana marehemu alitumia uhai wake wote katika kuitangaza Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kweli Leo SERIKALI zetu zinashindwa kutowa hata gari ya maana kupakia mwili wa Marehemu. Mwili wake umepakiwa kwenye pick up Kama mzigo wa kuni. Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi Ameen. Hatukumthamini wakati wa uhai wake na sasa Amefariki tumemfanya Kama mzigo wa kuni. Shame on Us

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.