Habari za Punde

Balozi Afungua Kiwanda Kipya cha Maji Zenj

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika uzinduzi wa kiwanda kipya cha maji ya kunywa hapo maeneo huru amani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifungua pazia kuashiria kukifungua rasmi Kiwanda cjha maji ya Kunywa cha Super Shine Kinachomilikiwa na Kampuni ya Safari yenye Makao Makuu yake Nchini India.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiangalia moja ya sampuli ya chupa ya maji yenye ujazo wa nusu lita ambayo tayari imeshakamilika utayarishaji wake katika kiwanda kipya cha maji ya kunywa kiliopo Maeneo huru Amani. 
  Balozi Seif akiwa pamoja na baadhi ya viongozi  wakishangiria moja ya nyimbo zilizokuwa zikiimbwa na kikundi cha sanaa kwenye hafla ya uzinduzi wa kiwanda kipya cha maji ya kunywa kiliopo maeneo huru ya Viwanda Amani.

 wasanii wa Kikundi cha sanaa Zanzibar wakitoa burdani safi katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda kipya cha maji ya kunywa kiliopo amani maeneo huru ya viwanda

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali na wale wa Kampuni ya Safari inayomiliki Kiwanda cha maji ya kunywa hapo amani eneo huru la Viwanda. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri anayesimamia Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Mh. Omar Yussuf Mzee, Mkurugenzi Mkuu wa ZIPA Nd Salum Khamis na Mmoja wa Viongozi wa Kiwanda hicho.Kushoto yake ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Safari inayomiliki Kiwadna hicho Bibi Mala Kalwan na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

2 comments:

  1. viongozi wetu vipi mshaomba vijipasenti kwenye hicho kiwanda, manaake kila mwekezaji akija basi kwanza akina sisi viongozi huomba vipasenti kama vile tumechangia kuanzisha hivyo viwanda, acheni tabia ya kujidhalilisha , wawekezaji wakija vitu vya kuangalia kuwa wananchi wetu wanapata ajira katika uwekezaji huo na sio kuangalia mafao binafsi

    ReplyDelete
  2. Hichi si kiwanda cha kujidai nacho serekali nzima na majisifu mengi kiwanda , kwa dunia ya hivisa karine ya 21 sikama mradi wa jua kali kwa wenzetu hopo Tanganyika kiwanda kama hiki hufunguliwa na diwani au mkuu wwiliaya, nyinyi viongozi wetu kutucheza shere sisi wananch,siku zina karibia bado miaka2 mtatuambi nini?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.