Na Masanja Mabula, Pemba
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka vijana kutodanganywa na wanasiasa kuwa watawapatia ajira.
Dk. Shein aliyasema hayo wakati akisalimiana na wanaCCM wa tawi la Kwale wilaya ya Micheweni katika ziara zake kichama kisiwani Pemba.
Alisema kauli hizo za wanasiasa hazina ukweli isipokuwa wanataka umaarufu na kutoa hadi za uongo na zisizotekelezeka .
“Sisi Serikali tumejiwekea utaratibu wetu, kwani tumeanzisha tume ya ajira ambayo ndiyo yenye mamlaka na uwezo wa kutangaza ajira, ule mtindo wa kujuana siku hizi haupo, cha msingi nawaombeni mujiajiri wenyewe kupitia vikundi vya ushirika,” alisema.
Aidha alisema serikali katika kipindi hichi imetangaza nafasi za ajira 2552 na vijana waliosoma kuanzia shahada ya kwanza , diploma na vyeti ni zaidi ya 7000, na kueleza kwamba serikali haiwezi kuwaajiri wote na kwamba njia ya kuweza kukabiliana na tatizo hilo ni kuanzisha vikundi vya ushirika .
Alisema Zanzibar ina maeneo mazuri yanayoweza kutoa ajira kwa vijana ikiwemo bahari kupitia uvuvi, kilimo na ushirika, ambapo endapo vijana watakaa pamoja na kuunda vikundi serikali itawasaidia.
Mapema Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika ,Haroun Ali Suleiman aliwataka wananchi katika wilaya ya Micheweni kujikusanya pamoja na kuanzisha vikundi vya ushirika vya uzalishaji mali ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na serikali.
Alisema serikali imeweka utaratibu mzuri wa kuwawezesha wananchi hasa wasio na mitaji ili waweze kukabiliana na ukali wa maisha na kwamba kupitia mikopo hiyo yenye masharti nafuu inampa uwezo mwananchi kujiajiri mwenyewe na kuacha kutegemea ajira kutoka serikalini.
“Kaeni mkao wa kula kwani serikali yenu itahakikisha changamoto zote zinazowakabili inazipatia ufumbuzi na muda mfupi wizara itawapatia msaada ambao utawezesha kuzimaliza changamoto zenu,” alisema.
Mimi nauliza na huenda ikawa suala hili lishawahi kuulzwa.
ReplyDeleteZiara hii ni ya kichama au ya kiserikali? naona ni mkorogo vyogo
Nasukuru kasema ukweli kuwa wao wanasiasa waongo na wanatoa ahadi zisizo tekelezeka kwahiyo hao walompa kura walietu
ReplyDeleteAti wasidanganywe na Wana Siasa.... Hii ahadi yakupatiwa kazi kwani siop yeye Sheni alipokua akitaka kura ilioahidi wananchi kuwapatia Wazanzibari kazi na kujenga Viwanda.
ReplyDeleteMbona Serikali yake Imeshinda kufanya hivyo?
Tulijua Zamanai san CCM kuendelea kutawala Wazanzibari kwamsaada wa Tanganyika itawafikisha Wazanzibari njia panda. Na sasa tunamuona Raisi Mzima anawaaambia Vijana kwamba Serikali haina kazi ila wajiajiri wenyewe na watapatiwa Mikopo.
Mikopo Gani hiyo inayotolewa na hao akina Masanja na Mabula? Wakisaidiana na Maskani za Kisonge?
Hapo kweli Mzanzibari hasa mwenye asili ya Pemba atapewa mkopo ? tumewaona nduguzetu ( Wapemba)wanaoingia SUZA, jinsi wanavyo nyanyaswa na Wahafidhuna pale Suza. Kwasababu tu wanatoka Pemba.
Mimi nawaona hao Wapemba wajinga wakubwa hata wakampokea huyo Kaburu Mweusi Vuai. Huyo ndie anaepiga Dbe nakuwataka Wapemba warudi makwao. Leo amejitia shati la kijani kama Nzi anakwenda kuchumbua mdomo wa Kimakunduchi. Mshezi mkubwa huyu..
Na Wapemba wameacha kazi wanasikiliza Utumbo.. Serikali gani hiyo ambayo inawaambia Wananchi hawana kazi.. au wasitegemee kazi? Basi bora pawe hapana serikali..
Wenzenu Watanganyika wanajenga Nchi yao na kuimarisha uchumi Wazanzibari ndio hao wanapiga vijembe nakukaa kwenye Viriri wakitisha watu nakuropokwa.
Kama hamuna ajira kwa vijana wa Pemba basi hamuna haja yakukusanya karafuu zetu...Utalii wenu si munao?
Naona kajigeuza kuku hunya na kula hapohapo
ReplyDelete