Hospitali ya kwanza ya kuzalisha Makunduchi ilijengwa na mwanamke wa Makunduchi Bi. Mwanayam Hija mwaka 1933.
Hospitali hiyo ilikuwa eneo liitwalo Mtegani karibu na Msikiti wa Ijumaa.
Kitendo hiki cha mwanamke wa Kimakunduchi kujenga hospitali ya kuzalisha kilitoa changamoto ya choyo cha maendeleo kwa bi. Sayyida Matuka, mke wa aliyekuwa sultan wa Zanzibar Seyyid Khalifa bin Hemed.
Bibi huyo alijenga hospitali ya kuzalia hapo eneo la Koba, Makunduchi.
Hospitali hiyo ilitumika kuzalishia watoto hadi ilipojengwa hospitali mpya ya Cottage. Hospitali iliyojengwa na Bi Matuka sasa inatumika kwa shughuli za kiutawala.
Katika picha upande wa kushoto anaonekana aliyekuwa sheha wa Makunduchi sheha Mzee na msaidizi wake, akifuatiwa na mkunga wa kizungu bi. Locket na mwanzilishi wa hospitali hiyo bi. Mwanayam ambaye nae alikuwa mkunga.
Habari na picha kutoka kwa ndugu Mohamed Muombwa
sawa sawa......
ReplyDelete