Habari za Punde

Kesi 134 zaripotiwa juu ya udhalilishaji wa wanawake na watoto Pemba

Na Abdi Suleiman, Pemba.
JUMLA ya kesi 134 za matukio mbali mbali ya udhalilishaji wa Wanawake na Watoto, zimeripotiwa katika kituo cha One Stop Center, kilichomo ndani ya Hospitali ya Chake Chake Pemba, tokea kuanza kazi kwake Julai 2 mwaka jana, hadi  April 2013 mwaka huu.
Kati ya kesi hizo kesi 77 ziliripotiwa kuanzia Julai 2 hadi Disemba mwaka jana, kati ya hizo kesi  22 ziko Mahakamani,  huku kesi 57 zikiripotiwa kuanzia Januari hadi Aprili mwaka huu, kati ya hizo kesi Sita tu (6) ndizo zilizoko Mahakamani.
Katika matukio hayo, kesi 52 za ubakaji wa wanawake na watoto, 38 kutoroshwea kwa mtoto aliyechini ya uangalizi wa wazazi wake, Saba (7) ni shambulio la Aibu, Tisa (9) Shambulio la kuumiza mwili , 18 kumpa mimba mtoti aliyekuwa hajaole na yuko katika uangalizi wa wazazi wake na kesi Kumi (10) kulawiti.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Maratibu wa kituo cha One Stop Center Pemba, Fatma Mohammed Salim, alisema kuwa katika ya kesi 77 zilizoripotiwa mwaka jana, kesi 32 za ubakaji, 23 kutoroshwa mtoto aliyechini ya uangalizi wa wazazi wake, kesi nane (8) kulawitiwa kwa watoto.
Aliendela kueleza kuwa, kesi Sita (6) ni shambulio la kuumiza mwili, kesi Nne (4) shambulio la aibu na kesi nne (4) kumpa mimba mtoto aliyechini ya uangalizi wa wazazi wake.
Kwa upande wa kesi 57 zilizoripotiwa Januari hadi Aprili 57 mwaka huu, Ubakaji ni kesi 20, 15 ni Kutorosha Mtoto aliechini ya uangalizi wa wazazi wake, shambulio la aibu kesi Tatu (3),  shambulio la kuumiza mwili kesi tatu (3), kumpa mimba mtoto aliyechini ya uangalizi wa wazazi wake kesi 14 na kulawiti kesi mbili (2).
Alifahamisha kuwa, bado Jeshi la Polisi limekuwa ni kikwazo kikubwa sana kwao, kwa kushindwa kuzifikisha kesi za ubakaji Mahakamani hali inayopelekea matendo hayo kuendelea kuiathiri jamii siku hadi siku.
“Inasikitisha sana kuona katika kesi 57 kesi sita tu, ndio zilizopelekwa mahakamani jee!  Hizo zilizobakia ziko wapi?aliuliza, kwa hali hii tutegemee kizazi kitakacho weza kuja kulipiza kisasi tu”alisema.
“hili jambo linaumiza sana kila siku, kuendelea kutokea kwa kesi hizi, hivi vyombo vya sheria viko wapi au ndio hawayaoni hayo matukio maana, tunasikia upelelezi hauonekani sasa lini upeleleza utakamilika”alisema.
Alisema kuwa, kipimo cha DNA kimekuwa ni kikwazo kikubwa sana kwao, hali inayopelekea hata baadhi ya wananchi kukatishwa taama, huku wazazi wakitaka kesi zao kufikishwa mbele kwenye vyombo vya sheria ili wabakaji kuchukuliwa hatua.
Aidha alisema kuwa, tayari jamii imeshaanza kuvunjika moyo kufuatiwa jeshi la polisi kushingwa kuwatia hatiani hata mtuhumiwa mmoja wa matendo ya ubakaji, yamekuwa ni kikwazo kikubwa kwao.
Hata hivyo, aliitaka serikali kuchangia fedha kidogo katika maabara ya Wawi Chake Chake Pemba, ili kuweza kukamilisha baadhi ya vipimo vya DNA, ambavyo tayari vipimo vidogo vidogo vipo katika maabara hiyo.
Kwa upande wake, Afisa Mdhamini wa Wizara Ustawi wa Jamii Maendelo ya Vijana Wanawake na Watoto Pemba, Mauwa Makame Rajab, alisema kuwa anasikitishwa sana na vyombo vya sheria kila siku zikizidi kushindwa kuwachukulia hatu watuhumiwa wa matendo ya ubakaji nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.