Kaimu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Abdilla Jihad, akihutubia katika maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Zanzibar yameadhimishwa katika ukumbi wa Hoteli ya Mazsons Shangani
Kaimu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Abdilla Jihad, akizinduwa Kitabu cha Ripoti kuhusu Mwenendo wa Vyombo vya Habari Tanzania ya mwaka 2012, wakati wa maadhimisho hayo yaliofanyika katika hoteli ya Mazsons Shangani.kulia Meneja wa MCT Tanzania Ofisi ya Zanzibar Suleiman Seif.
Kaimu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Abdilla Jihad akionesha ripoti hiyo kwa waandishi wa habari baada ya kuizindua.
Meneja wa Udhibiti na Viwango wa MCT Pili Mtambalike, akihutubia katika maadhimishohayo ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani. 
Meneja wa MCT Suleiman Seif akitowa maeleo ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons shangani.
Waandishi wa habari wakifuatilia madazinazowakilisha nawatoa mada hizo katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru Vyombo vya Habari Duniani huadhimishwa kila mwaka April 3.jumla ya mada mbili ziliwakilishwa. katika maadhimisho hayo.
Mtoa ya Mada ya kwanza katika maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC Redio, Rafii Haji aliwasilisha mada ya Kuhusu Vyombo vya Habari vya Umma katika Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa. Tanzania.
Mtoa Mada ya Pili Mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Ally Saleh, akitowa mada kuhusu Haki na Kupata Habari ni Suluhisho la Usalama kwa Wanahabari.
Waandishi walipata fursa ya kuchangia na kutowa mawazo yao kuhusu Mada hizo zilizowakilishwa katika Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.
ndugu Ally saleh , hakika upo katika nafasi nzito kimajukumu kwa mola wako , ya kwenye tume ya katiba, uweke mbele maslahi ya wznz, ambao hawataki muungano , na wewe ni tegemeo letu kwenye hilo ,pamoja na Nd Awadh , wengineo hatuna imani nao , msije kurubuniwa na kuiuza znz kwa watanganyika hakika adhabu ya Mungu itakuwa kali juu yenu kuliko hao wengine kwani hao wanajulikana ni wanafiki na ndio maana wakawekwa ktk tume. Msije kutuangusha , iwe bora kwenu kuhatarisha maisha yenu kwa kuitetea znz kuliko kukubaliana na kuunganisha katiba, MUUNGANO MWISHOOOOOOO
ReplyDelete