Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akisalimiana na Wanavikundi vya Ushirika wa Wanaweke Mkoani Pemba akiongoza ziara ya Wake wa Wawakilishi na Wbunge kutembelea Vikundi vya Wanawake na kutowa misaada katika vikundi hivyo.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akimkabidhi mmoja wa Wanavikundi vya Ushirika vya Mkoani fedha taslim Shilingi laki nne, kwa ajili ya kuendelea vikundi hivyo vya Kinamama,Fedha hizo zimetolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Balozi Seif na Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM, jumla ya Vikundi Sita vimefaidika na msaada huo katika Wilaya ya Mkoani Pemba.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akimkabidhi Mwanachama wa Kikundi cha Tuishi kwa Usalama cha Mkoani Tatu Mohammed Ussi, mkopo wa shilingi laki tano uliotolewa na kikundi hicho kwa Mwanachama wake. wakati wa ziara ya Umoja wa Wake wa Viongozi waCCM, Wilaya ya Mkoani Pemba.
Wanavikundi vya Ushirika wa Wanawake Wilaya ya Mkoani wakimsikiliza Mke wa Makamu wa Pili swa Rais wa Zanzibar akitowa nasaha zake kwa Wanaushirika hao, katika ukumbi wa Umoja ni Nguvu.
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa Maua Daftari na Bihindi Hamad wakisikiliza risala ya Wanaushirika.wakati wa kutowa misaada kwa Vikundi vyao katika ukumbi wa Umoja ni Nguvu Mkoani.
WANAUSHIRIKA wakishangilia katika mkutano wa kukabidhi misaada iliotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein na Umoja wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge kwa vikundi hivyo.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi akitembelea vikundi vya Ushirika vya Wanawake wa Wilaya ya Mkoani , baada ya kukabidhi michango yao kwa Vikundi hivyo katika Ukumbi wa Umoja ni Nguvu Mkoani.kuangalia bidhaa mbalimbali zinazizalishwa na Vikundi hivyo.
Kwanini wakopeshwe pesa badala yakugaiwa? Mbona Vikundi vya Unguja Hugaiwa Mamilioni ya pesa za Walipa kodi na Misaada.. Kwasababu CCM wanachukua pesa ya Serikali nakuitumia katika sherehe zao za kichama.. Siri imetoka.
ReplyDeleteSerikali ya Muungano Tanganyika/ Tanzania ndio hutiliana saini na Miradi ya Kimaendeleo katika sektor mbali mbali kama za ujenzi wa barabara, maji, umeme, kilimo n.k. Fedha hiyo huletwa kwaajili ya matumizi ya Serikali, lakini CCM huzichota nusu wakawa wanazitumia kwakuimarisha Chaa chao kizidi kutawala kimabavu.