Habari za Punde

Makamanda wataoshindwa kuwakamata wachochezi kutimuliwa

Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi amewaagiza Makamanda wa Polisi Mikoa, Wilaya na Wakuu wa vituo nchini, kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria watu wote wanaotumia majukwaa ya dini kukashifu dini nyengine.
Akinukuu msemo wa Kiswahili kuwa ‘ukicheka na Kima utavuna mabuwa’, Dk. Nchimbi alisema serikali haitacheka tena na watu wanaotaka kuitumbukiza Tanzania katika migogoro ya kidini, na kusema yeyote atakaefanya hivyo sasa atakamatwa.
Aliwaonya watendaji hao wa polisi kwamba watafukuzwa kazi, iwapo serikali itasikia kwenye mkoa, wilaya au kituo kuna matukio hayo huku viongozi hao wakishindwa kuchukua hatua.

“Tukisikia kwenye eneo lako matukio haya yamefanyika bila ya kuchukua hatua, utakwenda na maji, hatuwezi kucheka na watu wanaochochea chuki na kutaka kutugawa,”alionya Dk. Nchimbi.
Aidha aliwaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii kujiepusha na lugha za chuki na uchochezi huku akisisitiza kuwa serikali imekubaliana na taasisi husika kuanza kuwakamata watu wanaotuma ujumbe mfupi wa simu (sms) unaochochea chuki.

3 comments:

  1. Safi sana mkuu, lazma tuwape moyo wenzetu, maafa sio ya upande mmoja.. ni yetu sote!

    Mungu awape subra wafiwa na awasaidie majeruhi wapone haraka...kwa uwezo wake!

    ReplyDelete
  2. Kama kweli serikali imedhamiria kuleta amani ya kweli nchini waanze na kuufugia mtandao wa JAMII FORUM.

    Huu ni mtandao wa CHADEMA ambao kazi yake kubwa ni kulaani, kudharau na kuwashambulia WAISLAMU kuwa hawana akili, hawakusoma ni magaidi, hawana ajira n.k.

    Dharau za namna hii ndio zimetufanya tuanze kuhoji vigezo vitumikavyo ktk utowaji wa elimu, ajira mbali mbali pamoja na nafasi za uongozi hadi wengine wapate kiburi cha namna hii!

    ReplyDelete
  3. Leo lisha tota mh, unasema hayo?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.