Na Mwantanga Ame
JAMII imetakiwa kujenga utamaduni wa kushirikiana katika mazingira tofauti kutokana na kuwepo dalili za kuanza kubaguana.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais, mama Asha Suleiman Iddi, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waislamu katika sherehe ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad, (SAW), iliyoandaliwa na wanawake wa CCM wilaya ya mjini Unguja yaliofanyika ukumbi wa mikutano wa mkoa huo Amani mjini Zanzibar.
Alisema dini ya kiislamu imekuwa ikikataza vitendo vya kubaguana lakini jambo la kushangaza baadhi ya watu wameanza tabia ya kuwabagua wenzao kwa kisingizio cha madhebu jambo ambalo ni kinyume na muongozo wa dini hiyo.
Alisema ni vyema waislamu wakaona kasoro hiyo na kuachana nayo.
“Matendo yetu hayafanani na aliyokuwa akiyafanya kipenzi chetu Mtume Muhammad (S.A.W), Mtume wetu alikuwa akipenda watu, alikuwa karibu na watu alikuwa akihimiza kufanya mambo mema leo sisi tunafurahia vitu ambavyo viko kinyume na matendo yake,” alisema.
Alisema kama waislamu wataanza kuvurugana watambue wanatoa mwanya kwa maadui wa kiislamu kupenyeza mambo yao.
Alisema mwenendo huo haufai kuendelezwa na ni vyema wanawake wa CCM wakaupiga vita.
Aidha aliwataka wanawake kujenga tabia ya kuwafunza mambo mema watoto wao ili waweze kuwa na maadili mema.
Maulidi hayo yalihudhuriwa na wanawake wa chama hicho wa wilaya ya mjini wakiwemo Wabunge na Wawakilishi Wanawake.
Ni mshangazo kweli mama asha nyinyi ccm ndio mnaobagua watu au huyaoni mabango yanayoandikwa na wanamaskani wenu? juu ya ubaguzi wa upemba na uunguja? Polisi wanayaona na hakuna anaesema kitu, raisi pamoja na kuwa ananasibishwa na pemba na yeye pia hasubutu kusema kitu kwani atawakera wahafidhina sasa mama unasema nini na unafanya nini?
ReplyDeleteHebu jirekebisheni nyinyi viongozi ambao ndio mfano kwa wanananchi, mtakaponyooka nyinyi wananchi kazi yao ni kuwafuata kwa yale mema mnayoyafanya. Chuki zote na ubaguzi ni nyinyi viongozi ndio mnaozipalilia kwa maslahi yenu.
MIE NASHANGAZWA NA KITU KIMOJA TU NA HII NCHI YETU HAWA WAKE WA MARAIS KWANI NI WANA SIASA AU VIONGOZI WA SERIKALI MANAAKE UTAONA SIKU HIZI MAMA ASHA, MKE WA KIONGOZI GANI SIJUI AKEMEA KITU FULANI NA KILA KIKAO YUPO MBELE, INABIDI SERIKALI IANZE KUANGALIA HILI KWASABABU SIONI KAMA HAWA WANATAKIWA WAINGIE KATIKA MAMBO YA SERIKALI SANA
ReplyDeleteSasa haoni kama na yeye kashiriki katika ubaguzi? Maulidi ni ya Kiislamu, sasa iweje yatayarishwe na wanawake wa CCM peke yao? Sasa hii sio kujitenga wenyewe anayoizungumza?Hapa ina maana kuwa wanawake ambao sio CCM hawakualikwa na wala hawawezi kushiriki.
ReplyDeletePia ukitaka kujua ubaguzi, basi hesabu kuna viongozi wangapi kwenye serikali au taasisi ambao wana asili ya Pemba. Wapemba wanaendelea kubaguliwa mpaka leo.