Na Fatuma Kitima,DSM
MKE wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mama Salma Kikwete amewataka wazazi na walezi kulea watoto kwa upendo na kuacha ukatili,ubaguzi na unyanyasaji dhidi ya kundi hilo.
Taarifa hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam hivi karibuni katika hafla ya kuadhimisha miaka kumi ya fao la elimu linalotolewa na Mfuko wa Pensheni na kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofaulu kidato cha nne.
Mama Salma alisema mtoto akilelewa kwa upendo bila ya kunyanyasa ataweza kupata muda wa kutosha kusoma na atafanya vizuri katika masomo yake.
Alisema kuna baadhi ya walezi wanawanyanyasa watoto na wengine hata kuwafanyia vitendo vya ukatili pindi, ikiwemo ubakaji na kuwachoma moto pale wanapokosea.
“Ni lazima tukemee vitendo vya ukatili kwa kuwa watoto ndio tegemeo na viongozi wa Taifa la kesho,”alisema.
Alisema ili kudhibiti vitendo hivyo jamii haina budi kuwalinda watoto na mifumo yote ya ubaguzi na unyanyasaji na kulelewa katika mazingira ya upendo.
No comments:
Post a Comment