Na Kauthar Abdalla
SERIKALI ya Ras al-Khaimah imetoa dola za Marekani milioni 1.5 kwa ajili ya uchimbaji visima 50 katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba hasa vijijini.
Lengo la mradi huo mkubwa na kusaidia juhudi za serikali kumaliza tatizo la huduma ya maji safi na salama.
Mwakilishi wa kampuni ya Rasgas kutoka nchi hiyo ya Falme za Kiarabu, Krikor Khssemjiap aliyasema hayo wakati akizungumza na Waziri wa Uwezeshaji Wananchi, Kiuchumi na Ushirika, Haroun Ali Suleiman ofisini kwake Mwanakwerekwe.
Zabuni ya ujenzi wa visiwa hivyo, imetolewa kwa kampuni ya Chimba Resource ya jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa kampuni hiyo, Aman Mw oria alisema visima 34 vitachimbwa Unguja na 16 kisiwani Pemba.
Alitaja maeneo yatakayofaidika na mradi huo kuwa ni mikoa ya Kaskazini, Kusini na Wilaya ya Magharibi kwa Unguja na Mikoa yote miwili ya Pemba.
Aidha baadhi ya vijiji yatajengwa matangi ya kuhifadhia maji ambapo kazi hiyo inatarajiwa kukamilika baada ya miezi miwili ijayo.
Nae Waziri Haroun ameitaka kampuni hiyo kukamilisha kazi ya uchimbaji wa visima hivyo kwa wakati,ili wananchi waanze kufaidika na huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment