Hivi karibuni kumejitokeza baadhi ya wanaotembelea ZanziNews na kuweka maoni na comments zenye matusi na kuchafua hali ya hewa kinyume na khulka za binadamu aliyepata malezi sahihi kutoka kwa wazazi wake.
Tunatoa tahadhari ya mwisho kwa wanaotoa maoni kwamba ikiwa hali hii itaendelea itatubidi tuyafanyie uhariri (moderate) maoni kabla ya kuyaweka na hii ni tahadhari ya mwisho kwani kabla hali hii ilijitokeza na tukatahadharisha pia.
ZanziNews inaruhusu maoni ya aina yoyote yenye kupongeza, kukosoa, kurekebisha, kusaili na kadhalika endapo tu mtoa maoni ataheshimu taratibu zetu na kujiheshimu yeye mwenyewe.
ZanziNews ina mwaka wa nne ipo hewani na hatujawahi kuzuia maoni kwani tulikuwa na thiqqa na tabia na utamaduni wa mzanzibari kutokuwa na jadi ya kutukana hadharani pia tumewaamini na kuwaheshimu wanaotutembelea kwamba ni watu wenye ustaarabu na wanaweza kukosoa bila ya kutumia lugha ya matusi na wakaeleweka.
Tuwe pamoja kujenga Zanzibar yetu bila ya kuchafuana au kutukanana na tujifunze kukosoa kwa lengo la kurekebisha (Constructive critisim) ambayo siku zote hujenga na wala haibomoi.
Endelea kututembelea na kutoa maoni.
Natoa shukran kwa hili tunamba hii iwe ukumbi wa kubadilishana mawazo sio matusi
ReplyDeletevile vile musikose kutembeleya www.beltelraas.blogspot.nl
ReplyDelete