Habari za Punde

Uchukuaji wa Fomu kugombea Nafasi ya Rais wa ZFA Wapamba moto

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchanguzi wa Mdogo wa Chama cha Mpira Zanzibar ZFA, Gulam Abdalla, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na harakati za Uchaguzi Mdogo wa ZFA kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa ZFA ilioachwa wazi na Mwenyekiti wake aliyejiuzulu  Aman Ibrahim Mkungu.
 
Jumla ya Wanamichezo 4 wamejitokeza kuwania nafahi hiyo. akiwemo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa ZFA katika miaka ya 2000, Ibrahim Raza wengine Abdalla Juma, Rajab Ali Rajab, na Ravia Idrisa. 
 
Usaili wao unategemewa kufanyika katika ukumbi wa VIP Amani na uchaguzi kufanyika mwezi wa Juni 8, katika hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.