Habari za Punde

Zantel yazindua promosheni ya ‘Kwangua na Ushinde’ kwa wateja wa Zanzibar

 Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel,Zanzibar, Mohamed Mussa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuzindua promosheni ya 'Kwangua na Ushinde', kushoto kwake ni Afsa Masoko wa Zantel, Zanzibar, Ibrahim Attas.
Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel, Zanzibar, Mohamed Mussa akionyesha moja ya zawadi zitakazowaniwa wakati wa uzinduzi wa promosheni ua' Kwangua na Ushinde'. Kulia kwake ni Awaichi Mawalla, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Zantel, na kushoto ni Ibrahim Attas, AfisaMasoko wa Zantel Zanzibar



Zanzibar-6/5/2013: Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, leo imezindua promosheni ya ‘Kwangua na Ushinde’ kwa wateja wake wake wa Zanzibar ikiwa ni katika juhudi zake za kuwazawadia wateja wanaotumia mtandao huo.

Promosheni hiyo kubwa ambayo mshindi wake atajinyakulia gari, itawazawadia wateja wengine zawadi za kila siku kama muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni moja, pikipiki aina ya Vespa, komputa ndogo (Huawei Media pads) pamoja na modemu za 3G.

Ili kushiriki katika promosheni hiyo, wateja wapya na wale wa zamani wa Zantel wanapaswa kuweka muda wa maongezi wa kuanzia shilingi elfu moja au zaidi ili kuingia kwenye droo hiyo.

Akizungumzia promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa, alisema promosheni hiyo inathibitisha nia ya kampuni hiyo katika kuboresha maisha ya wateja wake huku wakiendelea kuwasiliana na ndugu na marafiki zao.

“Tuna furaha kubwa leo kuzindua promosheni hii kwa wateja wetu, ambayo hakika itawapa thamani ya pesa zao kwa kujishindia zawadi mbalimbali’’ alisema Mussa.

Promosheni hii itaendeshwa kwa kipindi cha miezi miwili, kuanzia leo tarehe 6 mwezi wa tano hadi tarehe 6 mwezi wa saba.

Kwa kipindi chote cha promosheni Zantel itatoa jumla ya modemu 60 za 3G, komputa ndogo 12 (Huawei Media pads), pikipiki 6, muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni moja pamaoja na gari moja.

“Promosheni hii itaipa kampuni yetu fursa ya kuwasiliana na wateja wetu, huku pia tukiwashukuru kwa kutumia huduma zetu’’ alisisitiza Mussa.

Wakati huo huo kampuni ya Zantel pia imetangaza kuzindua ofa mpya kwa wateja wake wa nchi nzima, iitwayo ‘Bonus Balaa’ ambayo itawapa mara mbili ya muda wa maongezi wakiweka vocha ya kuanzia shilingi elfu moja au zaidi.

Muda huo wa maongezi utawawezesha wateja wa Zantel kupiga mitandao yote.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.