Habari za Punde

Balozi wa Oman Nchini Tanzania Atembelea Jengo la Kiwanda cha Uchapaji Maruhubi.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.Mohammed Aboud, akiwa na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Yahya Moosa Al Bakry, akitembelea kuona ujenzi wa Jengo jipya la Kiwanda cha Uchapaji cha Serekali katika eneo la maruhubi kujionea ujenzi wake  
 Mtaalamu wa usimamizi ya ujenzi huo akitowa maelezo kwa Balozi wa Oman Mhe. Yahya Moosa Al Bakry, alipokuwa akitembelea jengo hilo wakiwa katika majengo ya kiwanda hicho maruhubi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud, akimuonesha michoro ya ramani ya ujenzi huo Balozi wa Oman Mhe. Yahya Moosa Al Bakry, wakati alipofanya ziara kujionea ujenzi huo wa awamu ya kwanza, ambapo sehemu ya kukaa mashine za uchapaji.   
Waziri Aboud akizungumza na Balozi wa Oman baada ya kukagua ujenzi huo, unaoendelea na ujenzi wake, Serekali ya Oman katika awamu ya Pili ya mradi huu itatowa msaada wa mashine kwa ajili ya kiwanda hicho kuboresha uzalishaji wake katika sekta mbalimbali za uchapaji.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.