Na Rose Chapewa, Morogoro
MIILI ya watu watano kati ya sita waliokufa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Maseyu Mikese Wilaya ya Morogoro barabara ya Morogoro -Dar es Salaam, imetambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao huku mmoja ukiwa bado haujafahamika na majeruhi watatu wakiwa bado wanaendelea na matibabu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa polisi mkoani hapa, John Laswai aliwataja kuwa ni Wafanyabiashara Tiu Mtega (35) na Exavery Haule (55) wakazi wa mkoani Njombe, Michael Japhet (40) mkazi wa Dar es Salaam, Juma Issack (32) mkazi wa Ilula mkoani Iringa na mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40 hadi 45 ambaye bado hajafahamika.
Aliwataja majeruhi kuwa ni Theresphory Mlowe (56) mkazi wa mkoani Njombe na Frank Rajab (50) mkazi wa Dar es Salaam ambao wote ni madereva wa magari yaliyongongana uso kwa uso katika eneo hilo pamoja na Azizi Kikoti aliyekuwa utingo.
Juni 1 mwaka huu saa 1:45 usiku katika eneo hilo gari namba T 957 AFJ scania iligongana uso kwa uso na gari namba T 855 BZW Mistubis Fuso na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi wawili ambao ni madereva wa magari hayo huku chanzo kikielezwa kuwa ni dereva wa lori kutaka kulipita gari lilokuwa limeharibika bila kuchukua tahadhari.
Katika eneo hilo na wakati huo dereva wa gari namba T417 BCN Mistubish Fuso Juma Issack alifariki dunia baada ya kugonga kwa nyuma gari jingine na hivyo kupoteza mwelekea kisha kugongana uso kwa uso na gari jingine na kusababisha kifo chake na majeraha kwa utingo wa gari hilo Aziziz Kikoti (24) chanzo kikiwa ni mwendo wa kasi.
Hata hivyo alisema majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro na kwamba wawili hali zao zinaendelea vizuri isipokuwa dereva mmoja ambaye bado hali yake si nzuri.
No comments:
Post a Comment