Habari za Punde

Usafiri wa Helikopta Dar - Kuondoa tatizo la msongamano!!!?

Kutokana na misongamano isiyo na tiba jijini Dar es Salaam, watu walionacho sasa wanatumia Helikopta kama muurubaini wa tatizo hilo la kuingia katikati ya jiji wakati mtu anaotaka, halikadhalika kutoka wakati autakao.
 
Helikopta hii ya kuingiza vibopa jijini imetua juu ya jengo la Holiday Inn Hotel, iliyopo mtaa wa Maktaba.
 
Usishangae kuona majengo mengi sasa jijini Dar yameweka vijiwanja vya helikopta na hivyo basi kuongeza idadi ya wanaosafiri kwa njia hiyo jijini. Picha na maelezo ni ndugu Mohamed Muombwa

1 comment:

  1. @ Kaka Mapara.

    Mambo kama haya munatakiwa nyinyi waandishi wa habari muyakemee na badala yakuandika reporti kama za kasuku.

    Viongozi wa Kiafrica hawana uongozi bora wala Imani na wananchi. Ati Headcopter hii inapandwa na Matajiri tu.. Why dont they not keeping it as an Air Ambulance. Ambayo ingeweza kusaidia na kuokoa maisha ya watu wengi sana... hasa ukiangalia ukubwa wa Nchi ya Tanganyika na jiji la DSM. Hakwishi kutokea ajali za mara kwa mara ambazo zinaua mamia ya wananchi kila siku.

    Wenzetu wa Nchi za Ulaya ( Au Nchi Zilizoendelea) Hutumia Headcopter kama hizo kwa Paramedic . Yaani kusaidia Wananchi wanaopata na Maafa kama ya Ajali za gari, mafuriko, mitetemekjo n.k.

    Huchukiliwa na Headcopter nakupelekwa hospitali ziliokaribu ili waweze kuokolewa maisha yao. Kwani mtu akipata ajali kama huku Jijini Dsm hata akifika hospitali ya Rufaa Muhimbili anakua tayari ameshapoteza damu au nguvu.

    Lakini kwetu sisi hakuna Uongozi bali Unyonyaji Mambo leo, Wanapanda Headcopter hiyo naamini ni wafanya Biashara, Mawaziri, na makatibu wakuu. Hawa wote ni walaji wa Mali za Umma ambao hawajali maisha ya Raia wa chini.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.