Habari za Punde

Uzinduzi wa Tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar limited Makunduchi


Jengo la Benki ya Watu wa Zanzibar Makunduchi Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Fedha Uchumi na Maendeleo Zanzibar Omar Yussuf Mzee akikata utepe kuashiria kulizinduwa Tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar katika Mkoa wa Kusini Unguja kushoto Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Amour na kulia Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho na Mwakilishi wa Makunduchi Haroun Ali Suleiman, wakishuhudia uzinduzi huo ikiwa ni sherehe za kutimia miaka 47 ya PBZ.  
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Maendeleo Omar Yussuf Mzee, akiwahutubia Wananchi waliofika katika sherehe za Uzinduzi wa Tawi jipya la Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ, baada ya kuzinduwa jengo hilo kwa ajili ya kutowa huduma za Kibenki kwa Wananchi wa MKoa wa Kusini Unguja   
Mkurugenzi Mkuu wa PBZ Juma Amour, akisoma risala katika uzinduzi huo na kutowa maelezo ya mafanikio ya PBZ hadi leo na malengo yake ya Baadae katika kupanua huduma kwa wateja wao waliokonje ya Zanzibar na ndani kwa kupata huduma zilizo bora na za uhakikika, ndio mafanikio iliopata PBZ  
Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa PBZ akitowa maelezo wakati wa sherehe hizo za uzinduzi wa PBZ katika Kijiji cha Makunduchi, uzinduzi huo umefanywa na Waziri wa Fedha Zanzibar Omar Yussuf Mzee,  
Viongozi wa Serekali wakimsikiliza Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa PBZ akitowa maelezo katika  sherehe hizo za uzinduzi zilizofanyika Tawini hapo Makunduchi.
 

Wananchi wa Kijiji cha Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja wakimsikiliza Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee, akihutubia wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tawi la PBZ Makunduchi, lilozinduliwa leo ikiwa ni shamrashamra za sherehe za maadhimishi ya miaka 47 ya Benki ya Watu wa Zanzibar. 
Mwananchi wa Kijiji cha Makunduchi akifunguwa Akaunti yake katika Tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar Makunduchi baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Fedha Zanzibar Omar Yussuf Mzee  

1 comment:

  1. Yaani pahala pakiwa hapana shughuli za kufanya utapajua tu,...SMZ yote iwa KAE?

    Kubwaa...ufunguzi wa tawi la PBZ, Waziri wa fedha na uchumi, waziri wa uwezeshaji, spika, Mkurugenzi mkuu wa PBZ, Msaidizi wake n.k

    Hapo ukiliza utaambiwa...'sisi waislamu'

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.