Mtume
Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam amesema:
{ أتاني جبريل فقال: يا محمد، عش ما
شئت فإنك ميت، وأحبب من شئت فإنك مفارقه، واعمل ما شئت فإنك مجزي به، واعلم أن شرف
المؤمن قيامه بالليل، وعزه استغناؤه عن الناس } [رواه الحاكم والبيهقي وحسنه
المنذري والألباني].
Alinijia Jibril
‘alayhis Salaam na akasema:
Ewe Muhammad; ‘ishi
utakavyo lakini (ujue) utakufa (na kuwa
maiti), mpende umpendae lakini (ujue) utatengana nae, fanya ufanyalo lakini
(ujue) utalipwa (kwa matendo yako) na utambue kwamba hadhi ya Muumin ( wa kweli
hutambulika) ni kusimama na kuuhuisha usiku na kusali na utukufu wake
(hujulikana) pale anapokuwa mbali na watu(akijiepusha na shari zao)
Imepokewa
Haakim na Bayhaqiy na Sheikh Albaani amesema ni hasan.
Hadithi
nyengine ya Ruwaza wetu na kipenzi chetu inayotuhimiza na kutusisitizia suala
zima la kusimama usiku na kusali na kutuonesha hadhi halisi ya aliyemuamini Allaah
Subhaanahu Wata’ala kikweli ni kwa kuacha kile anachokipenda ( kustarehe na
usingizi au na ahli yake) na kujipinda na kujibidiisha na ibada wakati ambao
hakuna mwengine anaemuona zaidi ya Allaah Subhaanahu Wata’ala (Ikhlaasi
iliyokamilika)
Mambo
ya kuzingatia na kukusaidia kukuwezesha kuuhuisha usiku na kusali Tahajjud
1 Kutokula
sana wakati wa kufutari ili mwili uweze kupata nguvu ya kutosha na kutochoka usiku.
2 Kutojishughulisha
sana mchana wa Ramadhaan na mambo yasiyokuwa muhimu kuuandaa mwili na Tahajjud
ili usichoke.
3 Kupata
muda mchana na kujipumzisha kwa kulala (Qayluulah) ili mwili usiwe mchovu
wakati wa usiku
4 Kujieepusha
na kufanya maasi mchana wa Ramadhaan kwani maasi humzuia mja na kuzifanya ibada
nzito
No comments:
Post a Comment