Habari za Punde

NBC wafutarisha


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akiongoza wananchi mbali mbali walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort jana

Wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC jana katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Rasort,wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis (hayupo pichani)akizungumza nao kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Shein

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania,Bibi Mizinga Mellu,akizungumza machache na kutoa salamu za Uongozi wa Benki hiyo wakati wa futari waliyoiandaa kwa wananchi wa Zanzibar jana katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,Wilaya ya Magharibi Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamohamed Shein,(katikati) na makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,wakiwa katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resort jana,(kulia)Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bibi Mizinga Mellu,na (kushoto) Mwenyekiti wa Bodi Dk.Mussa Assad

Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi,akisoma Dua baada ya kumalizika kwa futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resort jana,kwa Wananchi wa mbali mbali na wateja wa Benki hiyo upande wa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamohamed Shein,(kushoto) akisindikizwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania Bibi Mizinga Mellu,baada ya kumalizika kwa futari iliyoandaliwa na Benki hiyo jana katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort nje ya Mji wa Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamohamed Shein,(kushoto)akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania Bibi Mizinga Mellu,(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,(kati) baada ya futari iliyoandaliwa na Benki hiyo jana katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort nje ya Mji wa Unguja

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.