Habari za Punde

Bakatwa Lataka Uchunguzi Kuhusu Ponda.

Na Mwandishi wetu
BARAZA la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limeunga mkono kauli ya Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu kwa kuitaka serikali kuchunguza kwa kina tukio lililopelekea kupigwa risasasi kwa mhubiri wa kiislamu, Sheikh Issa Ponda.

Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Al Had Musa Salum alisema ingawa BAKWATA limekuwa likipingana na misimamo ya Sheikh Ponda, lakini serikali ilikuwa na nafasi ya kumkamata Ponda kwa kufuata mkondo wa sheria.

Sheikh huyo ambaye amekuwa katika mivutano ya mara kwa mara na serikali alidaiwa kupipigwa risasi baada ya kutokea vurugu mjini Morogoro.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Taasisi za Kisilamu,Mussa Kundecha, alisema endapo serikali haitachukua hatua itakayowaridhisha Waislamu, wataamua kufikiria upya mustakabali wao na serikali ya Tanzania.

Sheikh Ponda amelazwa katika hospitali ya taifa, Muhimbili, mjini Dar es Salaam akiuguza jeraha linalodaiwa kuwa la risasi huku akiwa chini ya ulinzi wa askari kanzu.

Msemaji wa Jeshi la polisi, Advera Senso amesema polisi kwa kushirikiana na jukwaa la haki jinai wameunda kikosi kazi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tukio hilo huku akikana kuwa Sheikh Ponda alipigwa risasi na polisi.

Senso aliwalaumu wafuasi wa Sheikh Ponda kwa kuwazuia askari kumkamata baada ya kuwarushia mawe; hatua iliyosababisha askari hao kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya na hata hivyo wafuasi hao walifanikiwa kumtorosha kiongozi huyo.

Taarifa za jumuiya hiyo ambayo inajulikana zaidi kama Shura ya Maimamu zinasema Sheikh Ponda ambaye polisi wanasema walikuwa wakimtafuta kwa tuhuma za kutoa matamko ya uchochezi, alisafirishwa usiku kutoka mji wa Morogoro hadi Dar es Salaam zaidi ya kilomita 200.

Sheikh Ponda kwa sasa anatumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja alichohukumiwa mapema mwaka huu baada ya kukutwa na makosa kadhaa ikiwemo uchochezi wa kuharibu mali za watu.

3 comments:

  1. Hapa shekh wa bakwata unajichanganya mwenyewe, ilikuwawa, huyu ponda aachekufanya fitna atetee uislam kwa busara na hikima sio kuchochea vurugu ambazo zitosababisha waislam na hata wasio weaislam kuumizwa sasa police washasema hawakumpiga risasi yeye ponda aseme kilomuumiza isiwe kajijeruhi mwenye ili apte huruma ya waislam akwepe sheria kwa uchochezi aloufanya, znz, umepelea wageni wetu kuhujumiwa kwa tindikali kwao tanganyika wametuli

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kijiwe usituchanganye kwanza wewe sio muislam wala mzanzibar kwa hiyo kaa kimua

      Delete
  2. Ili niwe mzanzibar niunge mkono ugaidi kama huu alikuja uanzisha huyu ponda hapa znz, kupeleka wageni wetu kumwagiwa tindikali, sisi tunajua muamsho wengi matajiri hawaja wahi kugawa hata penseli siunguja wala pemba wao kazi yao kuhamasisha fujo,ikesha wanataka tupumue, wasikie hutuwezi kupuma znz yetu ikawa pepo ya magaidi tunataka tupumue karaha mastarehe zanzibar daima

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.