Habari za Punde

Kombeni wailalamikia Mamlaka ya maji ZAWA

11.07zawa
 
Na Hamida Maulid {ZJMMC}
Wananchi wa Shehia ya Kombeni Wilaya ya Magharibi  wameilalamikia  Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kutokana na tatizo la maji linaloendelea kuwakabili kwa kipindi cha mwaka   mmoja  sasa  na kusababisha  kuzorotesha harakati zao za kiuchumi.
 
Wakizungumza na waaandishi wa habari wananchi wa shehia  hiyo, wamesema upungufu maji katika vijiji  vingi vya shehia hiyo na kuongeza  ugumu   wa maisha  kwa wananchi wengi. 
 
Wamesema  maji  yamekuwa yakipatikana   kidogo sana  na baadhi ya vijiji  hayatoki  kabisa  na wamevitaja vijiji hivyo kuwa ni  Kombeni  hospitali, Kombeni  branji  na Komboni michenzani.
“Maji yanatoka  kiduchu kiduchu sisi hatupati, na  tukipata ni kidogo sana na kwa muda mdogo  na hayana muda maalumu”. alifahamisha mwanakijiji wa Kombeni  branji bi. Afua  Abdalla kwa masikitiko.

Sheha wa shehiya ya Kombeni  Mussa Khamis Mussa  amesema  tatizo la maji lipo kwa muda mrefu na linawakabili baadhi ya wananchi wake licha ya juhudi aliyofanya ya kuwafuata  maafisa wa ZAWA  ili kutatua ufumbuzi wa tatizo hilo. 
 
Sheha Mussa  amesema    amewafuata  wahudumu  wa maji  katika kisima cha Dimani ambacho ndicho wanachotumia na kuelezwa  kwamba  mashine inayo tumika  katika kisima hicho  hivi sasa ni moja  tu   na  yapili  imeharibika na  ndio ililiopelekea upungufu wa maji katika shehia hiyo.
 
 Kutokana na kasoro hizo sheha ameiomba Mamlaka ya Maji  Zanzibar   kuwasaidia  mabomba  mengine ya maji ili kuyafunga katika kisima chengine cha Kombeni  kwa ajili ya kupunguza  tatito hilo la muda mrefu.
 
 Hata hivyo Afisa uhusiano wa ZAWA  Zahor Suleiman Khatib  amekanusha  kuharibika kwa mashine katika kisima cha Kombeni na wamesema  kisima hicho kina mashinei tatu na zote zinafanya kazi.
 
Zahor amewatupia lawama wananchi wanaounga maji   kiholela bila kufuata   taratibu  za Mamlaka na baadhi ya wakulima wanaotumia maji mengi  kumwagilia  mashamba yao  jambo ambalo linapelekea ukosefu wa maji katika baadhi ya vijiji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.