Wachezaji wa Zamani wa Timu ya Malindi na Taifa ya Zanzibar aliosimama Ali Shariff Adoff na Amour Azizi Kijeba. wakisubi mpambano huo, baada ya kutowa damu kupima Malaria.
Wachezaji wa timu mbili za Wachezaji wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Zanzibar na Taifa Stars wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza kwa mchezo wao.
Kikosi cha timu ya Jozani Veterani wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa Uzinduzi wa Mradi wa Malaria Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan, kikosi hichi kilikubali kufungwa na Maveterani wezao kwa bao 1--0.
Kikosi cha Maveterani cha Ngezi wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa Uzinduzi wa Mradi wa Malaria, ilitowa kipigo kwa Maveterani wezao wa Jozani kwa bao 1--0.
Wachezaji wa Veterani wakipasha kabla ya kuaza kwa mchezo wao.
Ingependeza zaidi iwapo kama tungefahamishwa majina yote ya mashujaa wetu hao waliocheza enzi zile ukifika uwanja wa Amaan saa 10.00 hupati nafasi ya kukaa labda iwe ni kwenye majukwaa ya kwenye magoli!!!!!! Hii hasa hasa ni kwa mechi zilizohusisha Small Simba, hahahahah aaaaa siku zimekwenda, je zitarudi??
ReplyDelete