WAKULIMA wa
zao la mwani katika kijiji cha Tumbe wilaya ya Micheweni kisiwani Pemba,
wanaendelea kukaa na mwani wao majumbani, baada ya kampuni ya Sea Weed,
kusitisha kununua zao hilo.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi kijiji huko, juu ya ukosefu wa soka la kuuzia mwani
wao, wakulima hao walisema kwa sasa wanalia njaa baada ya kampuni hiyo
kusitisha ununuzi.
Walisema ni
muda wa miezi mitatu sasa tokea kampuni hiyo ilipoingia mitini jambo ambalo
limekuwa likiwakosesha usingizi hasa kwa vile tayari wanao mwani mwingi wa
kuuza kwa kampuni hiyo.
Walisema
ukosefu wa soko unawatiwa hofu na unasababisha kuishi maisha ya kubahatisha.
Mmoja kati ya
wakulima hao, Abdallah Haji Juma alisema ana kiwango kikubwa cha mwani nyumbani
mwake, unaofikia magunia nane.
Nae Raya Salim
Ali alisema kutokana na kutonununuliwa kwa zao hilo kwa kipindi hichi chote,
hali ya maisha imekuwa ngumu.
‘’Ilikuwa maisha yanakwenda vizuri maana hata kwa
mahitaji yetu madogo madogo sio lazima kumsubiri baba, ilikuwa tunajikumu
lakini kwa sasa tumedorora,” alisema.
Mkulima
mwengine wa zao hilo, Salama Juma Ali, alisema zao la hilo kwa sasa limekuwa
vigumu kuendelezwa kwani kampuni inayonunua zao hilo haijawapitia wakulima kwa
kipindi chote hicho.
Meneja wa
Seaweed Cooperation,Hamial Said Soud, alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema
walisitisha kutokana na kuwa na mwani mwingi kwenye maghala yao.
No comments:
Post a Comment