Baraza la Katiba, Zanzibar (BAKAZA)
Press Release
Marekebisho ya Sheria ya Katiba Mpya Maoni ya Baraza la Katiba, Zanzibar (BAKAZA),
28 Septemba, 2013
Baraza la Katiba, Zanzibar (BAKAZA), ambalo ni jumuisho la asasi saba za kiraia*limesikitishwa sana na matukio katika Bunge la Tanzania siku ya Alhamis tarehe 5 Septemba2013, ambayo siyo tu yamevunja heshima ya chombo hiki cha uwakilishi wa Watanzania,bali yametishia kuvuruga kabisa mchakato mzima wa kuandaa Katiba Mpya inayotarajiwa naWazanzibari na Watanzania kwa ujumla.
Bunge la nchi ni kama kioo cha nchi yenyewe, na sura ilioonekana siku ya tarehe 5Septemba 2013 katika kikao cha Bunge kilichotaka kuupitisha Mswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mwaka 2013 kwa mabavu ya uwingi waWabunge wa upande mmoja, na amri ya Naibu Spika kuamrisha Mkuu wa Kambi yaUpinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe, kutolewa Bungeni kwa nguvu, ni aibu si kwaBunge tu bali kwa Watanzania wote.
1.
Ushirikishwaji wa Wazanzibari
Kazi kubwa lililopewa Bunge la Tanzania wakati huu ni kusimamia mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya kidemokrasia ambayo, kwa mara ya kwanza, ilitakiwa kuwashirikishawananchi wote, wa Zanzibar na wa Tanganyika. .
Katika kazi hii, Bunge limeonekana limeshindwa kabisa kumudu kazi yake kwa njia ya uwazi na ya kidemokrasia.
Ulipopelekwa Bungeni mswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mara ya kwanza Machi,2011, Bunge liliamuwa kuipeleka rasimu hiyo kwa wananchi. Kama tunavyokumbuka, Mhe.Samuel Sitta alipelekwa Zanzibar kwa makusudi ya kuiuza rasimu hiyo, lakini ilioibuka nisio tu wananchi hawakushirikishwa katika uundwaji wa rasimu hiyo, bali hata SMZilihadaiwa.
Tuligundua kwamba rasimu ya sheria ilipelekewa kwa SMZ, na kwa nia safi,SMZ iliijadili na kutoa mapendekezo kumi na nne. Kamati ya Bunge ya Katiba sio tuikachukua mawili tu na ikatupa mengine katika debe la taka, bali ikaendelea kuzidisha mambo mengine mengi bila kushauriana na SMZ.
Hii ilikuwa ni dharau kubwa kwaZanzibar na Serikali yake, na sote tunakumbuka namna ambavyo Zanzibar iliupokea mswada huo ambapo wananchi waliungana na Serikali yao kufika hadi Mswada ule kuchanwa hadharani.----------------- *
Zanzibar Law Society (ZLS), Waandishi wa Habari za Maendeleo ya Zanzibar (WAHAMAZA), ZanzibarYouth Forum (ZYF), Umoja wa Walemavu Zanzibar (UWZ), Zanzibar Female Lawyers’ Association(ZAFELA), Tanzania Media Women Association, Zanzibar (TAMWA), na Pemba Press Club (PPC) .
Inastaajabisha sana kwamba Bunge limesahau tukio hilo baada miaka miwili tu na kurudia makosa yaleyale ya kupitisha sheria zinazohusu mambo ya Muungano bila ya kuishirikishaZanzibar ambayo ni mshirika mwenza katika Muungano.
Tumeambiwa hadharani na Mhe.Abubakar Khamis, Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar, kwamba safari hii SMZilipelekewa Mswada unaorekebisha vifungu vinne tu, na wakaipitia na kurekibisha ipasavyo.Makamo wa Pili wa Rais, Mhe. Seif Ali Idi akapokea ripoti iliyotumwa kwake na MheAbubakar akishirikiana na Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na yeye Makamo wa Pili akaituma kwa Waziri Mkuu wa Muungano, Mhe. Pinda.
Lakini, ulipopelekwa Bungeni,mswada ulikuwa na vifungu 11 ambavyo vingi ya vifungu hivyo viliingizwa baada yaMakamo wa Pili kupeleka ripoti yake. Kitendo hichi kimefanywa kwa makusudi kuwadanganya Wazanzibari na Serikali yao na ni kitendo cha dharau ya mwisho kwamshirika mmoja wa Muungano kumfanyia mshirika mwenziwe.
Vitendo kama hivi ndivyovilivyopelekea wananchi wa Zanzibar kuona kwamba Muungano huu hauwatendei hakiWazanzibari bali pia unaidhalilisha SMZ kwa kiwango cha kuitia aibu mbele yaWazanzibari.
Kwa kuwa uundwaji wa Katiba lazima ushirikishe wananchi wa pande zote mbili, basi haikutosha Serikali ya Muungano kushirikiana na SMZ tu (hata kama ushirikishwaji wenyewe ni wa kisanii), bali walipaswa kuwashirikisha wananchi wa Zanzibar pia. .
Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba ilijua hivyo, na ilikutana na asasi za kiraia za Tanganyika lakini Kamati hiyo haikuona haja ya kukutana na hata asasi moja kutoka Zanzibar. Ingawa baadhi ya Wajumbe wa Kamati walisisitiza kutaka kufika Zanzibar na fedha kwa ajili hiyo zilikuwepo, lakini Kamati ya Bunge haikufika Zanzibar; hii ni jeuri na kibri wanayofanyiwa Wazanzibari kama kwamba wao si sehemu muhimu ya Muungano wa Tanzania.
Ubaya wa kutoshirikishwaji katika majidiliano juu ya marekibisho ya Sheria ya Katiba ni kwamba wananchi hawakuweza kutoa maoni yao juu ya masuala muhimu ya kikatiba yaliobadilishwa kwa haraka haraka, na kwa kiasi kikubwa, yanapunguza uhalali wa Katiba ijayo.
Hii ni kinyume na azma ya Rais Kikwete alipotangaza uanzishaji wa mchakato mzimawa kuandika Katiba Mpya ya kwanza kwa ridhaa ya wananchi tarehe mosi Januari, 2011.
2. Kupitisha Katiba Mpya Mbali na ushirikishwaji wa Wazanzibari katika mchakato wa kupata Katiba Mpya, suala lapili muhimu sana katika mchakato huu ni kupata ridhaa ya wananchi kwa uwingi (consensus)ili nchi isigawike baadaye.
Katika dunia nzima, na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yenyewe ilivyokiri katika kifungu cha 26, ili Katiba iweze kupitishwa katika Bunge Maalum, itahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya idadi ya wajumbe kutoka Tanganyika na idadi hiyo hiyo kutoka Zanzibar.
Kinyume chake, sheria sasa imerekebishwa kuonesha kwamba Katiba nzima kwa ujumla itapigiwa kura mara ya kwanza kutazama kwamba inapata theluthi mbili ya pande zote mbili;na kama haipati, basi Mwenyekiti wa Bunge Maalum ataorodhesha mambo yanayokosa ridhaa ambayo yatapigiwa kura mara ya pili mbali mbali; na kama itashindikana kupata theluthi mbili ya pande mbili basi, na hapa ndio Bunge limeteleza kikatiba kukubali nusu ya Bunge tu (simple majority) kupitisha mambo yalioshindwa kupata ridha ya theluthi mbili ya wajumbe kutoka kila upande.
Sasa hii inawafanya wapuuzi (stupid) wale wote waliodhani kuweka theluthi mbili ni kulinda maslahi muhimu kwa Washirika wa Muungano.Kama kifungu hiki kilihitaji kurekebishwa, basi ilikuwa kueleza mchakato wa kupitisha huo Katiba wa mpango wa busara na hekima, kuipitia ibara kwa ibara ili kila ibara iweimejadiliwa na imepata theluthi mbili pande zote mbili, na mwisho wake kupitisha Katiba nzima kwa uwingi hitajika, lakini sio kubadilisha msingi muhimu wa kikatiba wa theluthi mbili. Kama sehemu moja ya Wabunge iliokosa kupata theluthi mbili itakuwa mkaidi, basi hawatakuwa na haja ya kupata maridhiano (compromise) wakijuwa kwamba mwisho wake wataweza kuipitisha kwa aslimia khamsini tu. Na pengine wataweza kupitisha sio ibara tu bali Katiba nzima kwa aslimia 50% tu. Hii haitakuwa Katiba ya maridhiano bali mtego tu utakaozaa mauaji mwisho wake.
3. Muundo wa Bunge la Katiba
Suala la tatu ni muundo wa Bunge Maalum la Katiba. .
Kifungu cha 22 kinaeleza kwamba Bunge litakuwa na
:a) Wabunge wote wa Bunge la Muungano, waliochaguliwa mwaka 2010 kabla ya kuletwa suala la Katiba Mpya, na tuonavyo sisi hawa wote hawana uhalali(legitimacy) ya kuwawakilisha Watanzania juu ya suala hili;
b) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar waliochaguliwa mwaka 2010 ambao nao vile vile hawana uhalali;
c) Wajumbe 166 wataoteuliwa na Rais kwa makubaliano na Rais wa Zanzibar.
Hali halisi ilioko sasa ni asilimia 72 ya Wabunge na Wawakilishi wanatoka chama kimoja ambacho kimeshatangaza msimamo wake juu ya suala la Katiba. Tayari kimemfukuza Mwakilishi mmoja ambae alikuwa na msimamo tofauti, na inaweza kutumia kanuni ya‘three-line-whip’ kuwalazimisha Wabunge hawa kufuata msimamo wa Chama hicho tawala,na kutishia kuwafukuza kwenye chama chao wale wataokataa kutii amri ya chama.
Katika hali hii ilikuwa haina haja kuandaa Katiba Mpya na kupoteza mabilioni ya shilingi ya wavuja jasho kama chama kimoja tu kitaweza kuamua mustakbali wa Katiba yetu, na ilikuwa hamna haja kabisa kupoteza muda wa Watanzania eti kwa lengo la kupata Katiba ya “wananchi wenyewe”.
Jambo la pili liliojitokeza sasa ni kwamba wale Wajumbe 166 watateuliwa na marais wawili ambao hao vile vile wanatoka kwenye chama kile kile kimoja. Baada ya Serikali ya Muungano kuukataa usawa katika Bunge la Katiba kati ya Zanzibar na Tanganyika, idadi hii ya 166 ikabuniwa kuipa Zanzibar angalau theluthi moja tu ya hawa 166 katika bunge lile,ikidaiwa kwamba Zanzibar bado itaweza kuzuia chochote katika Katiba kwa sababu kutakuwa na kanuni ya theluthi mbili katika kupitisha Katiba.
Sasa tumeshaona kwamba theluthi mbili sasa imeyayuka, na Zanzibar haina kinga tena, kwa sababu, pamoja na theluthimoja ya hawa 166 wataoteuliwa na Rais wa Zanzibar, jumla ya Wazanzizbari wote katika
Bunge la Katiba watakuwa asilimia 36 tu, na chochote watachotaka kupitisha Watanganyika
mapande mawili makubwa.

basi wataweza kukipitisha bila khofu. Hapo tutaanza “Kero za Shirikisho.”
Lakini bado liko suala la vipi hawa 166 watateuliwa na marais wawili. Marekibisho ya Sheria
iliopitishwa na Bunge hivi karibuni inaeleza kwamba makundi yaliyotajwa katika kifungu
cha 22 (NGOs, asasi za kidini, vyama vya siasa, taasisi za elimu ya juu, makundi ya
walemavu, jumuiya za wafanyakazi, wakulima, na ya wafugaji, n.k.), yataalikwa
kupendekeza majina tisa ambamo marais watateua watatu kutoka kila kikundi. Katika hali
halisi tulionayo, bila kuwatilia shaka wataoteua hawa wajumbe, itakuwa vigumu
kuwahakikishia wananchi na vyama vya siasa vya upinzini na kuridhika, kwamba maslahi na
matakwa ya ubinafsi hayatotumika. BAKAZA lilipendekeza kwamba makundi haya ndio
wanayojuwa nani wanaweza kutetea maslahi yao katika Bunge la Katiba, na ni bora
kuwaachia wawachague wawakilishi wao wenyewe, kama ni watatu, basi wawe watatu, na
haina haja marais kuwachagulia.
Kwa vyovyote vile, hata hawa wajumbe 166, ambao theluthi moja tu ndio watatoka Zanzibar,
na wakijumuishwa na Wabunge wa Muungano na Wawakikilishi kutoka Zanzibar,
hawatobadilisha ukweli kwamba Bunge Maalum la Katiba bado litahodhiwa na chama
kimoja kwa zaidi ya theluthi mbili. Kwa bahati mbaya, namna Bunge lilivyotenda kazi yake
na kupitisha mswada wa marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba bila kuijadili kwa
undani, inaondowa matumaini kabisa kwamba Wabunge hawa wataweza kusimamia
upatikanaji wa Katiba Mpya ambayo itakuwa ya kidemokrasia na ya uadilifu. Ndio maana
BAKAZA ilipendekeza kwamba Wabunge wa Bunge Maalum wangechaguliwa kwa kazi
maalum ya kuandika Katiba tu ili kupata ridhaa (mandate) ya wananchi juu ya aina ya Katiba
wanayotaka wakati huu, na kuepuka matatizo tunayopata sasa. Na kwa sababu Katiba
tarajiwa ni ya Muungano wa nchi mbili zilizoungana 1964, basi ingetakiwa kuwa na
Wabunge sawa ili Mshirika mmoja asione anaonewa kwa udogo wake wa ardhi, uchumi au
idadi ya watu wake.
4. Kuuliwa kwa Tume ya Katiba
Katika mchakato wa kupata Katiba Mpya, kazi kubwa imefanywa na Tume ya Marekibisho
ya Katiba iliyoundwa mwaka 2011. Tume hii ni chombo peke yake kilichoheshimu usawa
kati ya washirika wawili waliounda Muungano 1964 kwa sababu kila upande ulitowa
wajumbe 15. Wajumbe wote hawa waliteuliwa na Marais wawili wa Muungano na wa
Zanzibar. Hesabu iliyofanywa na wadadisi wa habari ilionesha kwamba kiasi thuluthi mbili
kati yao walitoka au walikuwa karibu na chama tawala, na wengi sana kati yao walikuwa
waumini wa Muungano wa Serikali mbili hapo mwanzoni. Lakini, baada kuwasikia wananchi
kote nchini kutoka Zanzibar mpaka Kagera, Kilimanjaro mpaka Songea, na kutathmini hali
halisi na matakwa ya wanachi wakati huu, wengi wao wameshawishika kwamba, kama
tunataka Muungano uendelee, lazima mfumo wa Muungano urekebishwe. Na ndio maana
wamependekeza mfumo wa Shirikisho la serikali tatu. Kwa kazi hii iliyokuwa si rahisi kwa
waumini wa serikali mbili, wajumbe wa Tume wameonesha ukweli na uadilifu mkubwa na
kwa hiyo wanastahiki kupongezwa sana na wananchi. Mhe. Rais Kikwete mwenyewe
aliwapongeza kwa kazi nzuri waliofanya kujaribu kutatua “Kero za Muungano.”
Lakini, kitu kilichowashangaza wananchi sana ni kuona Tume hii chini ya Mhe. Warioba,
ambaye alikuwa karibu sana na Mwalimu Nyerere, na aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu na
Jaji, na hata Waziri Mkuu chini ya Rais Nyerere na Ali Hassan Mwinyi, sasa inalaumiwa eti
kutaka kubomoa Muungano kwa kupendekeza mfumo mbadala wa Muungano. Ushabiki wa
kichama ulitawala sana katika Bunge lililopitisha Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba mwanzoni mwa mwezi wa Septemba, 2013.
Chini ya kifungu 20 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba iliyopitishwa mwaka 2011, baada
kukamilisha Rasimu ya Pili na kuwasilisha kwa Rais, Tume hii ilikuwa inategemewa kutoa
ufafanuzi utakaohitajika wakati wa majadiliano katika Bunge Maalum, na pia kuwaelimisha
wananchi juu ya suala la Katiba Mpya na Kura ya Maoni itakayopigwa kukamilisha
mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya. Baada ya kupata uamuzi wa wananchi ndio Tume
hii ilikuwa ivunjwe chini ya kifungu cha 37 cha Sheria hiyo.
Lakini, namna Rasimu ilivyowakera Wabunge kadhaa, na kutumia hoja ya nguvu waliokuwa
nayo katika Bunge la sasa, wameamua kuiuwa Tume mara tu baada ya kuwasilisha Rasimu
ya Pili! Hata hivyo, wamelazimika kukubali chini ya kifungu 20(4) kwamba bado watahitaji
msaada wa Mwenyekiti, Makamu wake au mjumbe wowote wa Tume kulisaidia Bunge la
Katiba baada ya kuvunjwa. Namna utashi wa kichama ilivyotawala majadiliano katika
Kamati ya Sheria na Katiba na katika Bunge lenyewe, Wabunge hawa wameugeuka uamuzi
wao wenye kupitisha makisio ya Tume hiyo ya Shilingi bilioni 32 muda mfupi tu kabla ya
Tume kuitoa Rasimu ya Kwanza.
Kwa ujumla, Bunge la Muungano limeonesha wazi wazi kwamba limeshindwa kuonesha
busara katika maslahi ya nchi ya muda mrefu katika suala la Katiba Mpya, na kwa kiasi hicho
limejionesha kwamba haliwezi kutegemewa kujali maslahi mapana zaidi ya ustawi wa nchi
hii. Kama Bunge hili ndilo litakuwa sehemu kubwa ya Bunge Maalum la Katiba, basi tamaa
gani tunaweza kuwa nayo kupata Katiba Mpya ya kidemokrasia ya karne ya 21?
5. Ombi kwa Mheshimiwa Rais Kikwete
Mheshimiwa Rais, Tarehe mosi Januari ya mwaka 2011, katika salamu zako kwa wananchi
wa Tanzania, ulitangaza azma yako ya kuipatia Tanzania Katiba Mpya ili iweze kuiongoza
nchi katika karne mpya. Kwa nia safi kabisa, ulionesha kwamba ulikuwa unatarajia Katiba
hiyo, kwa mara ya kwanza katika nchi yetu toka kupata uhuru, iwe imewashirikisha
wananchi wenyewe katika uundwaji wake. Kwa dhamira nzuri kwa nchi yetu, sisi hatuna
budi tukupongeze na tukushukuru kwa kuonesha njia vizuri.
Katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya, sasa hivi tuko kwenye njia panda; ama
tutekeleze azma yako ya kuwa na Katiba ya demokrasia iliyopatikana kwa njia ya
kidemokrasia na iliowashirikisha wananchi wote, au kutumika hoja ya nguvu Bungeni, na
kwa makusudi kuwapuuza wananchi wa sehemu moja ya Muungano huu. Ni dhahiri kwamba
“Kero za Muungano” ndizo zilikuwa sababu kubwa ya kuhitajika Katiba Mpya. Kama
tutapotea njia wakati huu, na kuendelea kuwapuuza wananchi wa Zanzibar mara nyengine
tena, si Serikali ya Mapinduzi tu, wala si asasi za kiraia tu, bali wananchi kwa ujumla, basi
tujitayarishe kufungua kitabu cha pili cha “Kero za Muungano.”
Zanzibar ilikuwa nchi huru kamili ilipoungana na Tanganyika mwaka 1964 katika Muungano
wa Tanzania, na inastahiki kuheshimiwa si kwa maneno tu bali kivitendo, pamoja na
kikatiba. Kama Katiba Mpya itashindwa kukubali usawa wa Zanzibar na Tanganyika katika
Shirikisho la Tanzania, basi Shirikisho hilo halitakuwa halali na halitadumu. Kwa miaka 50
ya Muungano, Zanzibar siku zote imekuwa ndugu mdogo mbele ya kaka yake. Miaka 50
imetosha kabisa kwa ndugu mdogo huyu kuwa baba kamili anaehitaji usawa na kaka yake
mkubwa. Zanzibar inahitaji usawa sio katika mchakato wa kuunda Katiba Mpya tu, lakini pia
katika Katiba Mpya na Shirikisho jipya linalotarajiwa kuundwa.
Katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya, Tume ya Katiba chini ya uwenyekiti wa Mhe.
Joseph Warioba, wewe mwenyewe ulikiri kwamba Tume ilifanya kazi nzuri ya kuwasikiliza
wanannchi nchi nzima, na kupendekeza Rasimu ambayo inajaribu kushughulikia mahitaji ya
kizazi kipya cha karne mpya, na kuacha nyuma “kero za Muungano” zisizokwisha. Tume hio
ilipangiwa kazi ya kuibeba Katiba mpaka mwisho wake kupata ridhaa ya wananchi katika
kura ya maoni, au tuseme, kura ya uamuzi, kwa sababu wananchi ndio wakutoa uamuzi wa
mwisho. Kwa hivyo, tumeshangazwa sana kuona kwamba Bunge la Tanzania limeamuwa
kuiuwa Tume hii mara tu baada ya kumaliza Rasimu ya Pili, bila kutoa sababu za maana au
sababu zozote.
Kwa kuwa na nia safi toka mwanzoni mwa mchakato huu, bado hatujachelewa tunayo nafasi
ya kujirekebisha kwa kujali hadhi, nafasi na haki sawa kwa kila mshirika wa Muungano
katika hatua zote zilizobakia kutengeneza Katiba Mpya yenye ridhaa ya pande zote mbili.
Ulazimishaji wa matumizi ya nguvu katika hatua yoyote ni kutoitendea haki demokrasia na ni
kinyume na maumbile ya Tanzania, taifa ambalo linajisifia kuwa ni la kidemokrasia.
Inawezekana Bunge limeteleza katika mabishano na mivutano ya kivyama, lakini uamuzi
wao wa haraka utaondoa uhalali wa Katiba tarajiwa. Kitu kinachohitajika sasa ni busara
kuliokoa jahazi lilioanza kwenda mrama. Tunakuomba Rais Kikwete kuirejesha Mswada wa
Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Bungeni kwa kufikiria zaidi, na
kuipa nafasi SMZ na asasi za kiraia za Zanzibar ili kupata ridhaa ya pande zote mbili za
Muungano. Tunakumbushwa wosia aliopewa Mwinyi Mkuu wa Unguja iliochongwa kwenye
ngoma yake iliopo Beit al-Ajaib, inayosema:
“Matendo yako ni kioo cha uongozi Hivyo wakusanye watu wenye muelekeo tafauti
Kwa sababu mtu wa busara huwajumuisha na kuwatosheleza watu wote.”
Kinyume chake, tunaogopa kufikiria madhara yanayoweza kuikabili nchi iliyogawanyika
mapande mawili makubwa.
ReplyDeleteKila mtu awe na katiba yake , tumeungana serikali, baadae chama bado hamjatosheka sasa na katiba mtauzwa wazima wazima